Pata taarifa kuu

Pembe ya Afrika: Marekani yatangaza vikwazo kwa wafadhili wa Al-Shabaab

Nairobi – Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya watu 16 yakiwemo makampuni katika pembe ya Afrika na Mashariki ya kati kwa tuhuma za kujihusisha na utakatishaji wa fedha kwa ajili ya wapiganaji wa Al-Shabaab.

Marekani imeliorodhesha kundi la Al-Shabaab nchini Somalia kuwa la kigaidi.
Marekani imeliorodhesha kundi la Al-Shabaab nchini Somalia kuwa la kigaidi. RFI-Swahili
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Washington, mtandao huo wa kibiashara ni sehemu ya kundi la kimataifa linalochangisha na kutakatisha fedha kwa ajili ya kundi hilo linalohusishwa na Al-Qaeda ambalo linaendeleza shughuli zake nchini Somalia.Tayari Marekani imeliorodhesha kundi hilo kama la kigadi.

Miongoni mwa makampuni yaliolengwa ni pamoja na ile yenye makao yake nchini Dubai,fintech Haleel Commodities LLC ilio na matawi nchini Kenya, Somalia, Uganda na Cyprus.

Kampuni ya mabasi ya umma nchini Kenya pia imetajwa kutoa usaidizi wa kiusafiri kwa ajili ya harakati za wapiganji wa Al-Shabaab.

Wapiganaji hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio mjini Mogadishu na maeneo ya vijijini.
Wapiganaji hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio mjini Mogadishu na maeneo ya vijijini. AFP - HASSAN ALI ELMI

Mwezi Novemba mwaka wa 2022, Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya wasambazaji wa silaha kwa ajili ya Somalia.

Al-Shabaab imekuwa ikipigana na serikali ya Mogadishu inayooungwa mkono na Umoja wa Mataifa kwa zaidi za miaka 16.

Licha ya wapiganaji hao kuondolewa katika mji mkuu wa Somalia na vikosi wa Umoja wa Afrika, wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika maeneo yalioko nje ya Mogadishu, wakiwalenga raia, wanasiasa na kwa wakati mwengine kulenga mji mkuu.

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud, alitangaza vita vikali dhidi ya wapiganaji hao mwaka wa 2023.
Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud, alitangaza vita vikali dhidi ya wapiganaji hao mwaka wa 2023. AFP - HASSAN ALI ELMI

Serikali ya Somalia, mwezi Agosti mwaka wa 2022 ilitangaza kuanzisha oparesheni kubwa dhidi ya wapiganaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.