Pata taarifa kuu

Senegal: Msamaha wa rais kutangazwa hivi karibuni

Nchini Senegali, siku ya tano ya kampeni kabla ya uchaguzi wa urais mnamo Machi 24, 2024. Msamaha wa rais unaweza kutangazwa na Rais Macky Sall siku ya Jumatano hii, Machi 13. Sheria hii ilipitishwa na wabunge wa Bunge la taifa wiki moja iliyopita na kuwasamehe watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu uliofanywa katika muktadha wa maandamano, ambayo yafanyika kati ya mwezi wa Februari 2021 na 2024.

Wafuasi wa muungano unaomuunga mkono Bassirou Diomaye Faye, mgombea urais wa upinzani, nchini Senegal, wakati wa kampeni za uchaguzi huko Dakar, Jumapili Machi 10, 2024.
Wafuasi wa muungano unaomuunga mkono Bassirou Diomaye Faye, mgombea urais wa upinzani, nchini Senegal, wakati wa kampeni za uchaguzi huko Dakar, Jumapili Machi 10, 2024. © SEYLLOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Tarehe ya mwisho ya siku sita ya kuwasilisha rufaa kwa uvunjaji wa katiba ikiwa imekwisha, msamaha huu wa rais unaweza kutangazwa leo na Rais wa Senegal, kwa mfano wakati wa Baraza la Mawaziri, ambalo litafanyika leo. Macky Sall ana siku nne, hadi Jumamosi, kutangaza sheria hii.

Matokeo ya kwanza, ambayo yatafuatiliwa kwa karibu sana: kuachiliwa kwa mgombea urais wa chama kilichofutwa cha PASTEF, Bassirou Diomaye Faye, lakini pia uwezekano wa mpinzani namba moja wa nchi - Ousmane Sonko.

Wote wawili wako kizuizini kwa madai ya kuhatarisha usalama wa serikali na kutoa wito wa uasi, miongoni mwa wengine. Ousmane Sonko pia alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kukashifu. Hatia ambayo inaweza kuondolewa na sheria hii ya msamaha.

Lakini kwa sasa, hakuna ratiba ya kutangazwa na kutolewa kwa sheria hii bado imethibitishwa. Hata hivyo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari na mwanzilishi wa Gazeti la Le Quotidien, Madiambal Diagne, mshirika wa karibu na mkuu wa nchi, "Macky Sall atatangaza msamaha huu leo", amesema kwenye mtandao wa X. Sheria ambayo itapelekea kuachiliwa kwa anasiasa hawa wawili wa upinzani kulingana na mwandishi huyu.

Mkutano kati ya Amadou Ba na Macky Sall

Siku ya Jumanne jioni pia ulifanyika mkutano ambao ulizua maswali mengi: ule wa mgombea wa muungano unaotawala, Amadou Ba, na Rais Macky Sall huko Dakar. Amadou Ba alikuwa akifanya kampeni katika mji wa Tivaouane, magharibi mwa nchi. Kisha akakatiza mkutano wake kwenda Dakar na kukutana na Rais Macky Sall.

Bado kidogo haijachuja kuhusu mahojiano haya, lakini kulingana na mjumbe wa msafara wake, Amadou Ba alianza tena kampeni yake Jumatano hii. 

Hii inapaswa kuleta uwazi kidogo katika kampeni hii ya uchaguzi, wakati katika siku za hivi karibuni, vyombo vya habari vya Senegal vimekuwa vikizungumza kuhusu mgombea wa serikali - Amadou Ba - kutengwa, na kampeni ambayo ilikuwa ngumu kuanza kutokana na kukosa kuungwa mkono na sehemu ya muungano wa wengi. Vyanzo vingine viliripoti bajeti na nyenzo za propaganda ambazo zilichelewa kutolewa.

Tangu alipoteuliwa, Amadou Ba hajapata kuungwa mkono kwa kauli moja ndani ya chama cha rais, APR, ambacho ndicho kikubwa zaidi katika muungano huo, na hivyo kusababisha kauli zinazokinzana ndani ya walio wengi. Siku ya Jumanne, wanachama wengine wa muungano wa BBY bado waliendelea kumuunga mkono mgombea wao Amadou Ba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.