Pata taarifa kuu

Angola: Watu wanaodaiwa kuwa 'wachawi' wafariki baada ya kumeza dawa ya mitishamba

Watu zaidi ya hamsini wanaoshutumiwa kwa "uchawi" wamefariki nchini Angola baada ya kulazimishwa kunywa mchanganyiko wa mitishamba ili kubaini kama wanafanya vitendo vinavyochukuliwa kuwa vya uchawi, kulingana na vyanzo vya ndani na polisi kwenye redio ya taifa siku ya Alhamisi.

Waangola wengi hukimbilia “wachawi” ili kutatua mzozo au kabla ya kufanya uamuzi. (picha ya kielelezo)
Waangola wengi hukimbilia “wachawi” ili kutatua mzozo au kabla ya kufanya uamuzi. (picha ya kielelezo) © AFP
Matangazo ya kibiashara

Waangola wengi hukimbilia kwa “wachawi” waliopewa mamlaka ya juu zaidi kulingana na baadhi ya imani, kutatua mzozo au kabla ya kufanya uamuzi. Vitendo hivi vinapingwa hasa na Kanisa katika koloni hili la zamani la Ureno lenye Wakatoliki wengi.

"Zaidi ya waathiriwa 50 walilazimishwa kunywa maji haya ya ajabu ambayo, kwa mujibu wa washauri wa jadi, yanathibitisha kwamba mtu huyo anafanya uchawi au la," amesema Luzia Filemone, ofisa mteule wa manispaa ya Camacupa (katikati), kwenye redio ya taifa ambapo idadi ya vifo imeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

"Idadi ya vifo vilivyohusishwa na unywaji wa kioevu hiki iliongezeka kutoka 30 hadi 50," mkuu wa polisi wa eneo hilo António Samba ameiambia redio ya taifa.

Hakuna sheria nchini Angola inayoadhibu rasmi "uchawi". Lakini kiutendaji, "waze wa busara" wanaochukuwa nafasi ya washauri ndani ya baadhi ya jamii wanashauriwa ili kubaini kama mtu ni "mchawi".

Mchakato huo unahusisha kuwafanya wale wanaoitwa "wachawi" kumeza kinywaji cha mitishamba kiitwacho "mbulungo." Kwa mujibu wa baadhi ya imani, mtu akifa baada ya kunywa maji hayo, basi inathibitishwa kwamba alikuwa akifanya uchawi.

"Ni tabia iliyoenea sana kunywa sumu inayodhaniwa kuwa kwa sababu ya imani ya uchawi," msemaji wa polisi wa mkoa António Hossi ameeleza kwenye redio, akionya juu ya ongezeko la hivi karibuni la kesi hizi katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.