Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Walinda amani 8 wajeruhiwa katika mapigano Sake

Mapigano yalianza tena Jumamosi, baada ya muda mfupi wa utulivu, kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali na washirika wao katika mji wa kimkakati wa Sake, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo walinda amani wanane walijeruhiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Walinda amani waliojeruhiwa walitumwa kama sehemu ya Operesheni Springbok katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.
Walinda amani waliojeruhiwa walitumwa kama sehemu ya Operesheni Springbok katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Bintou Keita, katika taarifa yake amelaani "shambulio dhidi ya walinda amani lililotokea Machi 16 huko Saké", mji unaozingatiwa kuwa kizuizi cha kimkakati kwenye barabara ya Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. "Walinda amani wanane walijeruhiwa, mmoja yuko katika hali mbaya," Bii Keita amesema.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Bi Keita amethibitisha kwamba kwa wiki kadhaa, "Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walitumwa kama sehemu ya Operesheni Springbok huko Kivu Kaskazini" ambapo MONUSCO na Jeshi la DRC, FARDC, "wanaongoza kwa pamoja operesheni hiyo.

Luteni Kanali Guillaume Ndjike, msemaji wa jeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ameshutumu "jeshi la Rwanda" kwa "kulenga ngome za MONUSCO huko Sake wakati wa mapigano" kati ya jeshi la Kongo na M23.

Baada ya siku chache za utulivu, mapigano yalianza tena katika mji huu ulioko kama kilomita ishirini magharibi mwa Goma, walioshuhudia walisema. Hata hivyo hali ya tulivu ilitawala Jumapili asubuhi, kulingana na mashahidi hao.

Chanzo cha usalama cha Kongo ambacho kiliomba kutotajwa jina kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba walinda amani hao walijeruhiwa katika mashambulizi ya makombora kutoka M23 yaliyodondoka kwenye kambi yao. Kwa mujibu wa chanzo hiki, tukio hilo lilitokea wakati makundi yenye silaha yanayoitwa "wazalendo" "yalipowavamia waasi wa M23", waasi hao walirusha makombora kwenye mji huo, ikiwa ni pamoja na "mawili kuanguka katika kambi ya MONUSCO, wilayani Mubambiro na kujeruhi baadhi ya walinda amani.

Tangu kuongezeka kwa mapigano karibu na mji wa Sake mapema mwezi wa Februari, maelfu ya wakaazi wamekimbilia Goma.

MONUSCO ambayo inakamilisha miaka 25 ikiwa nchini DRC, ambayo ina walinda amani 15,000, ilianza kujiondoa nchini humo mwishoni mwa mwezi wa Februari. Mamlaka ya Kongo ilitaka zoezi hilo la kuondoka nchini DRC likamilike mwishoni mwa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.