Pata taarifa kuu

RDC: Maelfu ya raia mashariki mwa nchi wameendelea kutoroka makazi yao

Nairobi – Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maelfu ya watu wanaendelea kuyakimbia makwao wakikimbilia kwenye kambi karibu na Goma, wakihofia usalama wao kutokana na vita vya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali.

Mbali na Goma, baadhi ya watu wamekimbilia katika maeneo ya Kanyabayonga.
Mbali na Goma, baadhi ya watu wamekimbilia katika maeneo ya Kanyabayonga. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa kupitia Tume inayoshughukikia misaada ya kibinadamu, ulisema kuwa watu 100,000 wameyakimbia makaazi yao kutoka kweye mji wa Nyanzale.

Mbali na Goma, baadhi ya watu wamekimbilia katika maeneo ya Kanyabayonga, Kaskaziini Magharibi mwa nchi hiyo huku wengine wakiamua kutafuta makaazi mapya pembezoni mwa Ziwa Edward.

Maelfu ya raia wa Mashariki ya DRC wanaishi katika kambi za wakimbizi kwa hofu ya kushambuliwa na makundi ya waasi.
Maelfu ya raia wa Mashariki ya DRC wanaishi katika kambi za wakimbizi kwa hofu ya kushambuliwa na makundi ya waasi. AFP - GUERCHOM NDEBO

Ijumaa iliyopita, Shirika la Msalaba Mwekundu lilionya kuwa iwapo vita vitaendelea hali ya kibinadamu itaendelea kuwa mbaya na sasa inaomba Dola Milioni 60 ili kuwasaidia raia walioathiriwa na vita vinavyoendelea.

Mwaka uliopita, Umoja wa Mataifa ulisema, karibu watu Milioni 7 waliyakimbia makaazi yao nchini DRC kutokana na mizozo wakiwemo Milioni 2.5 katika jimbo la Kivu Kaskazini, hali ambayo inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.