Pata taarifa kuu

Niger: Hali itakuaje baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kijeshi kati ya Niamey na Washington?

Uhusiano wa nchi hizo mbili ulikuwa umezorota, lakini mpasuko sasa unaonekana kukamilika kati ya Niger na Marekani. Siku ya Jumamosi Machi 16, Niamey  ilivunja makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Washington, ambayo ina takriban wanajeshi elfu moja nchini humo, pamoja na kituo kikuu cha ndege zisizo na rubani huko Agadez. Ushirikiano "usio wa haki", "kutokidhi matarajio", na uwepo wa Marekani ni "kinyume cha sheria" utawala wa kijeshi umebaini.

Kanali-Meja Amadou Abdramane akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Niger, Julai 26, 2023. (Picha ya kielelezo)
Kanali-Meja Amadou Abdramane akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Niger, Julai 26, 2023. (Picha ya kielelezo) © Capture-écran ORTN.NE
Matangazo ya kibiashara

Haishangazi, Patriotic Front for Sovereignty (FPS), muungano unaounga mkono jeshi, umekaribisha "uamuzi wa kijasiri". Kulingana na muungano huo, mikataba hiyo ilivipa uwezo "wa kupita kiasi kwa vikosi vya kigeni". FPS inakwenda mbali zaidi na kutoa wito wa kufunguliwa kwa kesi za kisheria kwa uhaini mkubwa dhidi ya wahusika wa mikataba hiyo, iliyotiwa saini mwaka wa 2012, chini ya utawala wa Mahamadou Issoufou.

Hii ni habari njema kwa uhuru wa nchi yetu. Serikali yetu inaelewa kuwa hakuna nchi inayoweza kuhakikisha usalama wa nchi nyingine. Kila nchi lazima ihakikishe usalama wake. Kila mtu anahitaji washirika, lakini ushirikiano unahitaji kila pande husika kunufaika, sio upande moja unufaike mwingine upoteze, amesema Slimane Ibrahim kutoka CNSP huko Agadez.

Hamid Amadou N'gadé analaani uamuzi wa "kiburi, kutokuwa na shukrani, kutowajibika na kutokuwa na uwezo". Kulingana na mshauri wa mawasiliano wa rais wa zamani Mohamed Bazoum, ushirikiano wa Marekani, kinyume chake, "umekuwa wa maamuzi". Anataja kuundwa kwa vitengo viivyohusika na masuala ya vifaa, utoaji wa vifaa vya kijeshi, mafunzo ya vikosi maalum, ujenzi wa kambi ya Agadez, kituo cha kisasa idara ya ujasusi, nk. Anasema, utawala unaongoza askari wake "kwenye kichinjio".

Niger inakuwa "jumba la maonyesho ya makabiliano kati ya mataifa yanayoshindana"

Kwa mujibu wa Moussa Tchangari, kumalizika kwa ushirikiano huu "haishangazi", lakini uamuzi huu umekuja "haraka zaidi kuliko vile tungeweza kutabiri". "Ni uamuzi ambao utadhoofisha zaidi uhusiano kati ya Niger na nchi za Magharibi kwa ujumla. Tunakuwa ukumbi wa makabiliano kati ya nchi zenye nguvu zinazopingana. Kwa upande mmoja, kuna Urusi ambayo inataka kushirikiana na Niger, na kuna mamlaka ya Magharibi ambayo imewekwa kando,” anaelezea katibu mkuu wa chama cha Alternatives Espaces Citoyens.

Kulingana na mwanahistoria Arthur Banga, sasa kuna hatari kubwa ya kuwaona Wamarekani wakiondoka Niger, hivyo kuwafungulia mlango Warusi na wanamgambo wa kundi lao la Wagner. Hasa tangu ushirikiano na Moscow umeimarishwa, na ziara rasmi za viongozi wa Urusi na Niamey katika miezi ya hivi karibuni.

Wazo, kwa Niger, sio kutengwa kwa kidiplomasia lakini mabadiliko ya mshirika wa kimkakati kwa kuelekea Urusi ambayo pia, kupitia Wagner, inajaribu kupata tena eneo hili la ulimwengu. Urusi inaendelea vizuri hadi sasa.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, Wamarekani waliiomba serikali ya kijeshi kuandaa kipindi kifupi cha mpito, wazo likiwa kwamba kurejea kwa haraka kwa utaratibu wa kikatiba kungeruhusu jeshi kuondoka na kukomesha maelewano kati ya Urusi na Iran. Lakini CNSP isingependa kusikia kwa njia hiyo. "Utawala wa kijeshi hauko tayari kuondoka mamlakani, hali ambayo inakera Washington. Lazima tutegemee hali kuwa ngumu zaidi,” amesema Arthur Banga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.