Pata taarifa kuu

Liberia: Aliyekuwa mbabe wa kivita ahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela

Nairobi – Mahakama nchini Ufaransa, hapo jana zilimuhukumu kifungo cha miaka 30 jela, aliyekuwa mbabe wa kivita nchini Liberia, Kunti Kamara, baada ya kumkuta na hatia ya makosa ya dhulma dhidi ya binadamu wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Kamara, mwenye umri wa miaka 49 hivi sasa, awali alikuwa amehukumiwa kifo wakati kesi yake iliposikilizwa kwa mara ya kwanza jijini Paris mwaka wa 2022
Kamara, mwenye umri wa miaka 49 hivi sasa, awali alikuwa amehukumiwa kifo wakati kesi yake iliposikilizwa kwa mara ya kwanza jijini Paris mwaka wa 2022 AFP - BENOIT PEYRUCQ
Matangazo ya kibiashara

Kamara, mwenye umri wa miaka 49 hivi sasa, awali alikuwa amehukumiwa kifo wakati kesi yake iliposikilizwa kwa mara ya kwanza jijini Paris mwaka wa 2022.

Katika ushahidi uliowashtua wengi, Kamara anadaiwa kula moyo wa mwalimu mmoja wakati wa vita hivyo ambapo ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulitekelezwa.

Aidha amepatikana na kosa la kukiuka haki za binadamu kwa kushindwa kuwazuia wapiganaji waliokuwa chini  yake kuwabaka wasichana wenye umri mdogo mwaka wa 1994.

Watu zaidi ya laki mbili waliuawa wakati wa machafuko yaliotokea katika taifa hilo la Afrika Magharibi kati ya mwaka wa 1989 na 2003.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.