Pata taarifa kuu

Zaidi ya raia 110 washikiliwa na 'wanajihadi' kwa siku 6 nchini Mali

Zaidi ya raia 110 wamezuiliwa kwa siku sita na watu wanaoshukiwa kuwa "wanajihadi" katikati mwa Mali, nchi ya Saheli iliyotumbukia katika mzozo mkubwa wa usalama, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu duru za ndani siku ya Jumatatu.

Vikosi vya jeshi la Mali, FAMA, vinaendelea kukabilian na mashambulizi ya wanajihadi nchini humo.
Vikosi vya jeshi la Mali, FAMA, vinaendelea kukabilian na mashambulizi ya wanajihadi nchini humo. © AFP - MICHELE CATTANI
Matangazo ya kibiashara

Raia hao walikamatwa Aprili 16 wakiwa ndani ya mabasi matatu na "wanajihadi" ambao walilazimisha magari na abiria wao kuelekea msitu kati ya maeneo ya Bandiagara na Bankass (katikati), kulingana na muungano wa mashirika katika mkoa huu ambao wanaomba kuachiliwa kwa watu hao pamoja na afisa aliyechaguliwa wa eneo hilo.

"Tunadai kuachiliwa kwa zaidi ya abiria 110 waliokuwa wakisafiri ndani ya mabasi matatu yaliyotekwa nyara siku ya Jumanne na wanajihadi," Oumar Ongoïba, mwanachama wa muungano huo, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

"Mabasi hayo matatu na abiria bado wako mikononi mwa wanajihadi," afisa mteule kutoka Bandiagara ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu, ambaye hakutaka kutajwa jina kwa sababu za kiusalama na kubaini kwamba idadi ya abiria wanaozuiliwani "zaidi ya 120". Uvumi wa jeshi la Mali kuwakomboa raia hawa wanaozuiliwa ulienea baada ya utekaji nyara huu.

"Uvumilivu wa mashambulizi"

Mnamo Aprili 19, muungano wa mashirika ya Bandiagara ulichapisha taarifa kwa vyombo vya habari ukilaani "kuendelea kwa mashambulizi ya kigaidi", "kuongezeka kwa idadi ya watu waliokimbia makazi yao" katika miji, na "kutochukua hatua kwa vikosi vya jeshi" katika eneo hilo.

Tangu mwaka wa 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na vitendo vya makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State, ghasia zinazofanywa na makundi yanavyotangaza kujilinda pamoja na ujambazi. Mgogoro wa usalama unaambatana na mzozo mkubwa wa kibinadamu na kisiasa.

Vurugu hizo zimeenea hadi katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger, na kuharakisha kuingia madarakani kwa tawala za kijeshi kupitia mapinduzi katika nchi hizi tatu. Mali, Burkina Faso na Niger zilivunja uhusiano na Ufaransa na kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi na kisiasa na Urusi, na kuunda Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES) mnamo Novemba, na kutangaza kujiondoa katika Jumuiya ya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Jeshi lililoko madarakani tangu mwaka 2020 nchini Mali liliahidi kuandaa uchaguzi wa rais mwezi Februari ili kutoa nafasi kwa utawala wa kiraia. Lakini Waziri Mkuu wa Mali aliyeteuliwa na jeshi, Choguel Kokalla Maïga, alitangaza mwezi Aprili kwamba serikali ya kijeshi itaandaa tu uchaguzi kwa nia ya kurejea kwa raia madarakani mara nchi itakapopata utulivu.

Kulingana na vyanzo vya usalama na ripoti za kibinadamu, ghasia ziliongezeka katikati mwa Mali katika robo ya mwisho ya mwaka 2023, na operesheni za kijeshi huko ziliongezeka sana katika kipindi hiki.

Licha ya operesheni hizi, makundi yenye silaha yanaendelea na mashambulizi yao katikati na kusini mwa nchi, hata karibu na mji mkuu Bamako. Mnamo mwezi Machi, jeshi la Mali lilitangaza kuwa limezuia mashambulizi matatu ya "kigaidi" ambayo yalilenga kituo cha forodha kilicho umbali wa kilomita mia moja kutoka Bamako na kambi mbili za jeshi kusini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.