Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika watoa wito kwa Mali kutoa mchakato wa mpito baada ya mapinduzi.

Umoja wa Afrika, unaitaka Mali kuweka wazi mpango wa mpito unaoeleweka, ili kurejesha uongozi wa nchi hiyo kwa raia, baada ya jeshi kuchukua madaraka tangu mwaka 2020.

Rais mpya wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goita (katikati), akiwa amesimama pamoja na wajumbe wa Mahakama ya Juu wakati wa hafla ya kuapishwa kwake mjini Bamako mnamo Juni 7, 2021.
Rais mpya wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goita (katikati), akiwa amesimama pamoja na wajumbe wa Mahakama ya Juu wakati wa hafla ya kuapishwa kwake mjini Bamako mnamo Juni 7, 2021. © Annie Risemberg / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Umoja wa Afrika inakuja siku chache baada ya wiki hii, uongozi wa kijeshi kuagiza kuahirishwa kwa shughuli zote za kisiasa nchini Mali kwa muda usiojulikana.

Jeshi lilisema uamuzi huo umekuja ili kuhakikisha kuwa, kuna utaratibu na usalama wa wananchi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Aidha, Umoja wa Afrika umelaani hatua hiyo ya jeshi na kusema, inarudisha nyuma harakati za demokrasia nchini Mali.

Viongozi wa kijeshi wameendelea kupata shinikizo za ndani na nje, tangu walipochukua madaraka, na mpango wa awali wa kuhakikisha kuwa uchaguzi wa urais unafanyika mwezi Machi lakini hilo halijafanyika.

Tangu mwaka 2012, nchi ya Mali imekuwa ikikabiliwa na utovu wa usalama, mizozo na kisiasa na hali ngumu ya kibinadamu hali ambayo imeendelea kusababisha wananchi kuishi maisha magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.