Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Mashirika ya kiraia yatoa wito kwa ICC kuchunguza hali ya usalama

Mashirika ya kiraia yanasema yanatiwa wasiwasi na hali ya kisiasa na usalama nchini Burkina Faso. Miungano ya mashirika ya kiraia yanatahadharisha na kutoa wito kwa mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, lakini pia Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji mengi ya raia nchini Burkina Faso na kunyimwa uhuru wa watendaji kutoka mashirika ya kiraia, vyama vya wafanyakazi na wanasiasa. 

Mwanajeshi wa Burkina faso akipiga doria katika mji wa Ouahigouya, katika mkoa wa Yatenga, tarehe 29 Oktoba 2018.
Mwanajeshi wa Burkina faso akipiga doria katika mji wa Ouahigouya, katika mkoa wa Yatenga, tarehe 29 Oktoba 2018. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa miungano hii wanaomba kwa dharura uchunguzi na kufunguliwa mashtaka kwa wanaodaiwa kutekeleza uhalifu huu.

"Kuna udharura," anatangaza mratibu wa Miungano inayozungumza Kifaransa ya ICC, Ali Ouattara. Miungano hii ya mashirika ya kiraia inatoa wito kwa mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuhusu hali ya Burkina Faso.

Katika barua iliyotumwa Hague lakini pia kwa wadau wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, miungano inayozungumza Kifaransa imeorodhesha mamilioni ya Waburkina Faso waliokimbia makazi yao, maelfu ya waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi lakini pia unyanyasaji unaofanywa na vikosi vya serikali au wasaidizi wao (VDP), bila kusahau baadhi ya visa vya uhalifu wenye asili ya kikabila uliofanywa katikamaeneo mbalimbali nchini Burkina Faso. Hii inahusu hasa utekaji nyara wa watu kadhaa wa kiraia au wa kisiasa, kulazimishwa kuandikishwa katika jeshi na mauaji ya raia katika vijiji vya Nodin na Soro yaliyotekelzwa Februari 25, 2024, ambapowatu wasiopungua 223 waliuawa kinyama.

"Ikikabiliwa na mzunguko huu wa kutokujali," waraka unasisitiza, "ni muhimu kwamba kesi za kisheria zianzishwe ili kuwakamata wahalifu na kutoa haki kwa waathiriwa," viongozi hao wa miungano ya mashirika ya kiraia. Kwa sasa huko Hague, Addis Ababa au New York, hakujawa na hisia zozote kwa tahadhari hii ya kumi na moja.

Hivi karibuni, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch lilisema jeshi la Burkina Faso liliua raia wasiopungua 223, wakiwemo watoto wasiopungua 56, katika vijiji viwili mnamo Februari 25, 2024.

Mauaji haya, ambayo ni miongoni mwa dhuluma mbaya zaidi kufanywa na jeshi nchini Burkina Faso tangu mwaka 2015, yanaonekana kuwa sehemu ya kampeni iliyoenea inayoongozwa na jeshi dhidi ya raia wanaotuhumiwa kushirikiana na makundi ya Kiislamu yenye silaha, na yanaweza kujumuisha uhalifu dhidi ya binadamu. Wanajeshi waliwaua watu 44, wakiwemo watoto 20, katika kijiji cha Nondin, pamoja na wengine 179, wakiwemo watoto 36, katika kijiji jirani cha Soro; vijiji hivi viwili viko katika wilaya ya Thiou, katika jimbo la Yatenga, kaskazini mwa nchi, lilibaini shirika la HRW.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.