Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Mtu mmoja afariki na wafanyakazi 47 wamekwama baada ya kuporomokewa jengo

Mwanamume mmoja amekutwa amekufa chini ya vifusi vya jengo lililokuwa likiendelea kujengwa ambalo liliporomoka siku ya Jumatatu huko George, kwenye pwani ya Afrika Kusini, na ambapo wafanyakazi 47 wamekwama, polisi imetangaza usiku wa kuamkia Jumanne.

Jengo la gorofa nyingi lililokuwa likijengwa katika mji wa pwani wa George nchini Afrika Kusini liliporomoka Mei 6, 2024, na wafanyakazi 48 wamekwama chini ya vifusi, mamlaka katika mji wa George imesema.
Jengo la gorofa nyingi lililokuwa likijengwa katika mji wa pwani wa George nchini Afrika Kusini liliporomoka Mei 6, 2024, na wafanyakazi 48 wamekwama chini ya vifusi, mamlaka katika mji wa George imesema. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Uchunguzi umefunguliwa baada ya mwili wa mwanamume huyo kupatikana chini ya vifusi," afisa wa polisi Christopher Spies amesema katika taarifa fupi.

"Kikosi cha wafanyakazi cha takriban watu 70 kilikuwa kwenye eneo la tukio wakati wa kuporomoka" kwa jengo hili lililokuwa likijengwa, muda mfupi baada ya saa 8:00 mchana, amesema msemaji wa manispaa Chantel Edwards .

Kati ya jumla hiyo, watu 22 walilazwa hospitalini, ameongeza, bila kutoa taarifa zaidi juu ya hali ya wengine ambao bado wako chini ya vifusi. Mario Ferreira, msemaji wa shirika lisilo la kiserikali la Gift of the Givers, aliyekuwepo kwenye eneo la ajali, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waokoaji "waliwasiliana na baadhi ya watu chini ya vifusi".

Jengo hilo la ghorofa tano, ikiwa ni pamoja na maegesho ya chini ya ardhi, liliporomoka kwa sababu ambazo bado hazijafahamika. Picha za maafa zinaonyesha eneo la ujenzi lililoboreshwa ambalo huduma nyingi za dharura zimewekwa. Paa la jengo linaendelea kuonekana juu ya rundo la kifusi.

George ni mji wa ukubwa wa wastani wenye wakaaji karibu 160,000, ulio karibu na Njia ya bustani ya kitalii, ambayo inapita kando ya pwani ya kusini ya nchi. Ukumbi wake wa mjini unaendeshwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo, Democratic Alliance (DA), ambacho pia kinatawala jimbo la Western Cape.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.