Pata taarifa kuu

Shambulio dhidi ya kambi Goma: DRC yataka Rwanda ichukuliwe vikwazo

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumatatu, Mei 6, Serikali ya DRC imeomba vikwazo vya kimataifa dhidi ya Rwanda, kufuatia shambulio dhidi ya kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na mji wa Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Shambulio hilo lililohusishwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Kigali, lilisababisha takriban vifo vya watu kumi na tano.

[Picha ya kielelezo] Kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya Mugunga, karibu na Goma.
[Picha ya kielelezo] Kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya Mugunga, karibu na Goma. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

"Jumuiya ya kimataifa ichukue haraka vikwazo vikubwa vya kisiasa na kiuchumi ili kuilazimisha Rwanda kuachana na matukio yake ya kigaidi na mauaji kwenye ardhi ya Kongo," inakumbusha Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kinshasa pia inasema inahifadhi haki ya kutoa mahitimisho yote kuhusu mchakato wa Luanda na inamtaka mwezeshaji "kuwajibika kwa hili". Mchakato huu, unaoongozwa na Rais wa Angola João Lourenço, unalenga kupata "suluhisho la mazungumzo" la mgogoro kati ya DRC na Rwanda.

Kwa hivyo Serikali ya Kongo inazungumzia mabomu yaliyorushwa na waasi wa M23, ambayo yaliua takriban raia 15 na kuwajeruhi wengine 35 siku ya Ijumaa Mei 3, kulingana na ripoti ya muda iliyochapishwa na mamlaka ya mkoa. Mabomu hayo yalilipuka katika eneo la Lushagala, lililopo katika kambi ya watu waliopoteza makazi yao katika wilaya ya Mugunga, magharibi mwa mji wa Goma.

Kinshasa inaorodhesha mfululizo wa mashambulizi mengine ya mabomu yaliyolenga raia katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita:

  • shambulio la bomu liliotokea Februari 2, 2024 huko Mugunga, karibu na shule ya msingi
  • shambulizi la bomu dhidi ya soko la Mugunga na kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Nzulo mnamo Februari 7, 2024.
  • shambulio la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Goma na ndege zisizo na rubani za Rwanda mnamo Februari 17, 2024
  • shambulio la bomu lililolenga raia huko Sake mnamo Februari 22, 2024
  • shambulio la bomu lililolenga raia huko Nzulo magharibi mwa Goma mnamo Machi 18, 2024.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.