Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Covid-19: Marekani yaondoa vikwazo vya usafiri kwa nchi za Kusini mwa Afrika

Kwa upande wake, Marekani imeondoa vikwazo vya usafiri kwa nchi nane za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini. Mwezi mmoja baada ya kupiga marufuku kwa mtu yeyote anayekuja kutoka kusini mwa Afrika ambako kirusi kipya cha Omicron kiligundulika, wasafiri kutoka ukanda huo wataweza kusafiri hadi Marekani kufikia Desemba 31.

Desemba 31, 2021, Marekani itaondoa vikwazo vya usafiri kwa nchi nane za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini. Mwezi mmoja baada ya kupiga marufuku kwa mtu yeyote anayekuja kutoka Kusini mwa Afrika ambako kirusi kipya cha Omicron kiligundulika.
Desemba 31, 2021, Marekani itaondoa vikwazo vya usafiri kwa nchi nane za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini. Mwezi mmoja baada ya kupiga marufuku kwa mtu yeyote anayekuja kutoka Kusini mwa Afrika ambako kirusi kipya cha Omicron kiligundulika. REUTERS - MIKE SEGAR
Matangazo ya kibiashara

Kudumisha vizuizi hivi kulishutumiwa kwani kirusi kipya cha Omicron kilikuwa chanzo kikuu cha maambukizi duniani kote.

Kwa nini kudumisha kizuizi hiki cha usafiri kwa nchi nane za Afrika (Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji, Malawi) wakati aian mpya ya kirusi cha corona cha Omicron sasa kimezikumba nchi nyingi duniani? Ikiwa ni pamoja na Marekani ambapo kirusi hiki kimekuwa chanzo kikuu cha maambukizi mapya nchini humo.

Swali hili limeshikiliwa mara nyingi na utawala wa Biden katika wiki za hivi karibuni. Maafisa kadhaa wa Kiafrika walishutumu vizuizi vilivyoendelea kama visivyo vya haki na visivyo vya lazima.

Omicron tayari ipo kwa wingi nchini Marekani

Mwanzoni mwa juma, wakati akizungumza juu ya Covid-19, rais wa Marekani alikumbusha kwamba utawala wake haujawahi kufikiria kufanya vizuizi hivi kuwa vya kudumu na kwamba alitathmini hali hiyo mara kwa mara na timu zake za 'wataalam wa kisayansi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.