Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-DPLOMASIA

Blinken kuzuru China kwa lengo la kufufua mazungumzo na Beijing

Marekani imethibitisha leo Jumatano Juni 14 ziara iliyosubiriwa kwa muda mrefu wikendi hii ya mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken kwenda China kufufua mazungumzo na Beijing.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba katika Ukumbi wa Jiji la Helsinki, Finland, Juni 2, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba katika Ukumbi wa Jiji la Helsinki, Finland, Juni 2, 2023. © via REUTERS / LEHTIKUVA
Matangazo ya kibiashara

"Bw. Blinken atakutana na maafisa wakuu wa China na kujadili umuhimu wa kudumisha njia wazi za mawasiliano ili kusimamia kwa uwajibikaji uhusiano wa China na Marekani," imesema taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, shirika la habari la AFP limeripoti.

Ziara ya Antony Blinken iliyokuwa imepangwa awali ilifutwa ghafla mwezi Februari.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa kuendelezwa mawasiliano wakati alipozungumza na Waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang.

Mazungumzo yao ya simu yamefanyika kabla ya mkutano wa ana kwa ana mjini Beijing. Blinken amesema kuwa Marekani itaendelea kutumia mazungumzo ya kidiplomasia ili kutatua wasiwasi wake pamoja na maeneo ya kuwepo na ushirikiano.

Naye Qin aliihimiza Marekani kuwacha kuingilia mambo yake ya ndani na kuuathiri usalama wake. Qin alimwambia Blinken aheshimu masuala ya msingi ya China kama vile suala la Taiwan ambayo China inasema ni sehemu ya himaya yake.

Mahusiano kati ya madola hayo mawili makubwa kiuchumi yamezorota katika miaka ya karibuni kuhusiana na suala la kisiwa cha Taiwan, biashara na haki za binaadamu, miongoni mwa mambo mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.