Pata taarifa kuu

Burkina Faso, Mali, Niger: Watu milioni 7.5 wako katika 'uhaba mkubwa wa chakula'

Watu milioni 7.5 kutoka nchi za Burkina Faso, Mali na Niger, wanakabiliwa na "uhaba mkubwa wa chakula", Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji ya Haki za Kibinadamu ya Marekani (IRC) imeonya Jumatatu.

A woman carries water on her head from a swamp, with much of the area having no access to clean drinking water due to years of unprecedented flooding, in Canal-Pigi County, South Sudan Thursday, May 4
Burkina Faso, Mali na Niger zimo kwenye orodha ya nchi 46 zenye maendeleo duni iliyotolewa na Umoja wa Mataifa. Kila moja ya nchi hii inaongozwa na wanajeshi walioingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi na zinakabiliwa na ghasia mbaya kutoka kwa makundi ya wanjihadi. AP - Sam Mednick
Matangazo ya kibiashara

"Kiwango cha uhaba mkubwa wa chakula na utapiamlo unaohusiana unaendelea kuongezeka katika ukanda huo. Katika eneo la Sahel pekee (Burkina Faso, Mali na Niger), watu milioni 7.5 wameathirika, ongezeko moja ikilinganishwa na milioni 5.4 mwaka jana," IRC imeandika katika taarifa kwa vyombo vya habari. Takriban watu milioni 70 wanaishi katika nchi hizi tatu.

Hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi katika nchi hizi, pamoja na Cameroon, Chad na Nigeria, kati ya mavuno, kuanzia mwezi Juni hadi mwezi Agosti. "Katika Afrika Magharibi na Kati, uhaba wa chakula umeongezeka hatu kwa hatua katika kipindi cha miaka mitano iliyopita," anasema naibu mkuu wa IRC katika kanda ya Afrika Magharibi, Modou Diaw, aliyenukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Majanga ya hali ya hewa yamezidisha" hali hii pamoja na "utapiamlo na ukosefu wa usalama", na "kusukuma vijana, wanaume na wanawake, kuhamia ndani na nje ya kanda hii", ameongeza.

Burkina Faso, Mali na Niger zimo kwenye orodha ya nchi 46 zenye maendeleo duni iliyotolewa na Umoja wa Mataifa. Kila moja ya nchi hii inaongozwa na wanajeshi walioingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi na zinakabiliwa na ghasia mbaya kutoka kwa makundi ya wanjihadi.

Baada ya jeshi la Ufaransa kukubali kuondoka kwenye ardhi zao, nchi hizo tatu zilikusanyika pamoja ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES). Walipata washirika wapya, ikiwa ni pamoja na Urusi. Siku ya Jumamosi, wakufunzi wa Urusi walipeleka mahitaji ya kimsingi nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.