Pata taarifa kuu
MAREKANI

CIA yatoa taarifa mpya kuhusu mtu aliyewezesha kuzua shambulio la bomu ndani ya ndege

Taarifa mpya kutoka nchini Marekani kuhusu mtu ambaye alisaidia majasusi wa nchi hiyo kumbaini raia ambaye alikuwa amepanga kulipua ndege moja ya Marekani alikuwa ni mmoja wa maofisa CIA na Serikali ya Yemen.

Umar Farouk Abdulmutallab, mtuhumiwa aliyetaka kulipua ndege ya Marekani
Umar Farouk Abdulmutallab, mtuhumiwa aliyetaka kulipua ndege ya Marekani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya usalama wa taifa nchini Marekani imesema kuwa mtu ambaye alifanikisha maofisa wake kuweza kumkamata mtuhumiwa aliyepangwa kulipua ndege hiyo alikuwa akifanya kazi kwa siri na mtandao wa Al-Qaeda ambao ndio ulikuwa umepanga njama hizo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa mtu ambaye alikuwa ametengeneza bomu hilo alikuwa ni raia wa yemen, Ibrahim Hassan Tali al-Asiri ambaye alilitengeneza kwa mtindo ambao vyombo vya usalama visingeweza kubaini mahali lilipo

Umar Farouk Abdulmutallab raia wa Nigeria ndiye aliyekuwa amebeba bomu hilo kwenye ndege ya Detroit siku ya sikukuu ya Krismas akiwa amevaa kifaa cha mlipuko kwenye nguo yake ya ndani na alikuwa amepanga kulipua ndege hiyo kabla ya kutua.

Akiwa kwenye harakati za kutaka kutekeleza shambulio lake, Umar alizuiwa na mmoja wa abiria kabla ya maofisa wa usalama wa Marekani hawajafanikiwa kuzima jaribio lake.

Bunge la Congress nchini humo limepongeza mtandao wa CIA kwa jinsi walivyowezesha kufanikisha kumbaini mtu ambaye angehusika na shambulio hilo na kutaka kuwa na maofisa zaidi kwenye makundi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.