Waziri Mkuu wa Tanzania, asema Magufuli yupo salama anaendelea na majukumu yake
Baada ya kutoonekana hadharani kwa wiki mbili na kuwepo kwa uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa rais wa Tanzania John Magufuli anaumwa, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Kassim Majaliwa amesema rais Magufuli yupo salama na anaendelea na majukumu yake kama kawaida.
Imechapishwa:
Akizungumza siku ya Ijumaa, Majaliwa alisema kulikuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu juu ya afya na alipo rais Magufuli katika siku za hivi karibuni huku watu kwenye mitandoa ya kijamii ndani nan je ya nchi hiyo wakiendelea kuuliza aliko rais huo aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Katika hili nataka kuonesha masikitiko yangu kwa baadhi ya watanzania ambao hawapendi maendeleo ya taifa letu wamejaa na chuki tu, wako nje ya nchi na wanatamani kuwachonganisha watanzania.
Aidha, Majaliwa amesema wanaomzushia ugonjwa rais Magufuli wanaongozwa na chuki.
Tangu juzi mpaka leo asubuhi tunaona watanzania wenzetu wenye husda wanashawishi vyombo vya kimataifa wasema rais wa Tanzania anaumwa, kajifungia, tena hata hawapo Tanzania wapo nje. Sisi tupo ndani lakini tupo kimya. Wanaona fahari kuisema nchi yao vibaya.
Soma zaidi hapa-Rais Magufuli yuko wapi ? Wapinzani nchini Tanzania wauliza
Mara ya mwisho kwa Magufuli kuonekana hadharani ilikuwa ni Februari 27 wakati akimwapisha Katibu Mkuu kiongozi na hata hakuonekana wakati wa kikao cha viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyoka kupitia njia ya mtandao.