Pata taarifa kuu
TANZANIA

Rais wa Tanzania John Magufuli aaga dunia

Rais wa Tanzania aliaga dunia Jumatano hii, Machi 17, akiwa na umri wa miaka 61, Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kwenye runinga ya taifa.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

 

John Magufuli, rais mzalendo mwenye kauli za kupinga masharti ya kudhibiti janga la Corona, hajaonekana hadharani tangu mwishoni mwa mwezi Februari.

Akilihutubia taifa usiku wa Februari 17, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisema Magufuli alifariki majira ya saa 12:00 jioni kutokana na tatizo la moyo.

Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa makamu huyo wa rais Magufuli alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa moyo kutoka hospitali ya Jakaya Kikwete.

Tanzania yapuuzia hatari ya COVID-19

Rais Magufuli alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa hawaamini uwepo wa ugonjwa wa COVID-19. Mwaka uliopita alisema Tanzania ilifanikiwa kupambana na kuudhibiti ugonjwa huo kupitia siku tatu za maombi.

Tangazo la kifo chake linajiri zaidi ya wiki mbili tangu alipoonekana hadharani na kuzua uvumi kwamba alikuwa akiugua virusi vya Corona.

Wakosoaji wanasema kupuuza kitisho cha virusi vya corona kulikofanywa na Marehemu Magufuli pamoja na kukataa kuweka masharti na kuchukua hatua za kuvidhibiti virusi hivyo kama yalivyofanya mataifa mengine huenda ikawa kumechangia vifo vingi nchini humo kikiwemo kifo chake mwenyewe. 

Tanzania haijaripoti visa au vifo vitokanavyo na corona tangu mwezi Aprili 2020. Lakini idadi ya vifo vya watu wanaokufa kutokana na matatizo ya kupumua iliongezeka mapema mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.