Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania yamuaga Magufuli Dodoma

Mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania John Magufuli unaagwa leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika na wananachi.

Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (C) akiondoka baada ya kuaga mwili wa haya rais wa Tanzania John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Tanzania Machi 20, 2021.
Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (C) akiondoka baada ya kuaga mwili wa haya rais wa Tanzania John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Tanzania Machi 20, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Asubuhi hii, mwili wa Magufuli unaagwa na wabunge, kabla ya kuelekea katika uwnaja wa Michezo wa Jamhuri ambako ataagzwa rasmi na viongozi mbalimbali ambao wameanza kuwasili nchini humo. Leo ni siku ya mapumziko nchini humo.

Maelfu ya wananchi walijitokeza usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Tanzania Dodoma kuupokea mwili wa aliyekuwa rais wao Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki tarehe 17.03.2021.

Marais wa nchi 10 na viongozi wengine wanatarajiwa kuhudhuria shughuli hiyo.

Magufuli ambaye alifariki dunia wiki iliyopita kufuatia matatizo ya moyo, atazikwa siku ya Ijumaa nyumbani kwake huko Chato.

Mwishoni mwa juma lililopita, maelfu walijitokeza jijini Dar es salaam kutoa heshima zao za mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.