Pata taarifa kuu
TANZANIA

Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na mtangulizi wake John Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 mwezi Machi.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la jeshi Machi 19 2021.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la jeshi Machi 19 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo mpya wa Tanzania, amemteua mwanadiplomasia wa muda mrefu Liberata Mulamula aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu Mkuu wa nchi za Maziwa Makuu ICGLR, kuwa Waziri mpya wa Mambo ya nje.

Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Palamagamba Kabudi,ambaye amehamishwa kwenye Waziri wa Sheria na Katiba.

Nimeona nimewabadilishe badilishe kwa sababu tangu mlipoapa si muda mrefu sana kwa hivyo ni vigumu kufahamu nani kafanya nini, lakini nawakumbusha kuwa hawa tunaanza nao awamu hii ya sita, tunapoendelea tutaona ni nani tutaenda naye na yupi tutamwacha njiani, nawaomba sana mkafanye kazi zenu.

Katibu Mkuu kiongozi Bashiru Ali, aliyekuwa ameteuliwa na Hayati Magufuli katika nafasi hiyo, ameteuliwa kuwa mbunge na nafasi yake imechukuliwa na Hussein Kattanga Balozi wa nchi hiyo nchini Japan.

Mabadiliko haya yamefanyika wakati wa kuapishwa kwa Makamu mpya wa rais Philip Mpango Ikulu ya Chamwino huo Dodoma.

Jawadu Muhammed mchambuzi wa siasa za Tanzania, ameimabia RFI Kiswahili kuwa mabadiliko haya yanaonesha kuwa, rais huyo mpya wa Tanzania, hatabiriki na anafanya maamuzi yake kwa usiri mkubwa.

Mawaziri wengine waliobadilishwa ni pamoja na Mwigulu Nchemba, ambaye anajaza nafasi ya Makamu wa rais wa Philip Mpango.

Waziri Ummy Mwalimu aliyekuwa Waziri wa  Muungano na Mazingira , sasa ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) huku aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo Selemani Jafo sasa atahudumu katika Ofisi ya Makamu wa rais.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.