Pata taarifa kuu
BURUNDI-JAMII

Burundi: Tume ya Ukweli na Maridhiano yatambua mauaji ya Wahutu mwaka 1972 na 1973

Nchini Burundi, Tume ya ukweli haki na maridhiano iliyoundwa mwaka 2014 kuchunguza chanzo na migogoro katika nchi hiyo, katika ripoti yake, imebaini kuwa chini ya utawala wa rais Michel Michombero kulifanyika mauaji ya kimbari dhidi ya kabila la wahutu mwaka 1972.

Moja ya vikao vua Bunge la Burundi.
Moja ya vikao vua Bunge la Burundi. AFP - ONESPHORE NIBIGIRA
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Ukweli na Maridhiano, ambayo iliwasilisha ripoti yake siku ya Jumatatu, Desemba 20 kwa mabunge yote mawili nchini Burundi ilibaini mojawapo ya matukio mabaya zaidi ya mauaji ya kikabila katika nchi hii ambayo yalianza mwishoni mwa mwezi wa Aprili 1972 kama "mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu katika miaka ya 1972 na 1973. Kwa leo Wahutu ndio wanashikilia madaraka. Mabunge yote mawili yaliidhinisha ripoto hiyo kwa vifijo na nderemo.

Tume ya Ukweli na Maridhiano, CVR, ambayo Iliundwa mwaka wa 2014, ilikuwa na kazi ngumu ya kuchunguza uhalifu uliofanywa katika nchi hii tangu Mkutano wa Berlin mwaka wa 1885 hadi mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 2008. Lakini CVR ilizingatia uchunguzi wake katika kipindi hiki cha kisichoelrweka.

Ripoti iliyowasilishwa kwa mabunge yote mawili yaiyokutana ni kubwa. Zaidi ya kurasa 5,000 ambazo ni muhtasari wa miaka ya uchunguzi zililenga zaidi kile ambacho Warundi hadi sasa wanakiita "matukio ya 72". Tarehe ambayo inaendana na mojawapo ya matukio mabaya zaidi ya mauaji ya kikabila katika nchi hii.

Mashahidi 900 waliohojiwa

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Pierre Claver Ndayicariye, CVR ya Burundi, kwa muda wote huu, imesikia takriban mashahidi 900 wakiwemo wale wanaodhaniwa kuhusika na mauaji hayo, tume ilifukua mabaki ya karibu wahanga 20,000 katika makaburi 200 ya pamoja, au hata kutafiti maelfu ya hati zinazohusiana na kipindi hiki.

Kulingana na Tume hii, inaibuka kutokana na uchunguzi huu kwamba "ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo wa haki za binadamu ambao uliwalenga Wahutu walio wengi mwaka wa 1972 na 1973" "ulipangwa" na mamlaka ya Rais Michel Micombero, kutoka jamii ya Watutsi walio wachache.

Pierre Claver Ndayicariye kwa hivyo "alitangaza rasmi Desemba 20, 2021 kwamba uhalifu wa mauaji ya halaiki ulifanywa dhidi ya Wahutu wa Burundi mwaka 1972 na 1973" tamko ambalo "lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu", amesema Spika wa Bunge, Gélase Daniel Nbabirabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.