Pata taarifa kuu

Kigali yaishutumu Kinshasa kwa kutaka kuachana na makubaliano ya amani ya Luanda

Rwanda imeishutumu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Alhamisi kwa kuachana na makubaliano yenye lengo la kuleta amani mashariki mwa DRC , eneo linalokabiliwa na matatizo ambayo yamezusha mvutano kati ya nchi hizo mbili jirani.

Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa kilele wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC.
Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa kilele wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC. AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Kigali imeshutumu DRC kwa kutaka "kuachana" na michakato ya amani iliyoanzishwa mjini Luanda na pia Nairobi.

"Majaribio ya DRC ya kuhujumu au kuachana na mikataba hii ya kikanda inaweza tu kuonekana kama chaguo linalolenga kuendeleza migogoro na ukosefu wa usalama," mamlaka ya Rwanda imesema katika taarifa.

Siku moja kabla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Christophe Lutundula alisikitika siku ya Jumatano kwamba waasi wa M23 "na mamlaka ya Rwanda inayowaunga mkono" "kwa mara nyingine tena, hawakuheshimu ahadi zao".

Serikali ya Kongo inathibitisha azma yake ya "kulinda uadilifu wa ardhi " ya DRC ambayo "itajilinda kwa njia zote", ameongeza. Licha ya matangazo ya kusitisha mapigano na kuondolewa kwa wanajeshi, mapigano yanaendelea mashariki mwa DRC kati ya jeshi la Kongo na waasi wa kundi la M23 ("Mouvement du 23 mars").

Mkutano wa kilele wa Novemba 23 huko Luanda hata hivyo ulikuwa umeamua kusitisha mapigano kuanzia Novemba 25, na kufuatiwa siku mbili baadaye na kuondolewa kwa M23 kutoka maeneo yaliyotekwa kwa miezi kadhaa katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

DRC inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono uasi huu hasa wa Watutsi ambao walichukua silaha tena mwishoni mwa 2021 na kupigana, jambo ambalo Kigali inakanusha. Kigali, kwa upande wake, inashutumu jeshi la Kongo kwa kushirikiana na waasi wa Kihutu wa Rwanda walioasisiwa mashariki mwa DRC tangu mauaji ya kimbari ya Watutsi mwaka 1994 nchini Rwanda.

Katika kujaribu kupunguza hali ya wasiwasi mashariki mwa DRC, ambayo imekuwa ikikumbwa na ghasia za makundi yenye silaha kwa takriban miaka 30, mipango kadhaa ya kidiplomasia imeanzishwa, hususan na Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC).

Mwishowe waliamua kupeleka kikosi cha kanda na kuanzisha kikao kipya cha mazungumzo ya amani mjini Nairobi mnamo Novemba 28, bila ya M23, ambayo Kinshasa inaelezea kama kundi la "kigaidi". Upatanishi mwingine unafanywa kwa niaba ya Umoja wa Afrika na Rais wa Angola Joao Lourenço, anayehusika na kujaribu kupatanisha Kinshasa na Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.