Pata taarifa kuu
UGANDA/UN - HAKI ZA BINADAMU

Uganda yasema haitatoa kibali kipya kwa ofisi ya haki ya Umoja wa Mataifa

Serikali ya Uganda imesema haitatoa kibali kipya kwa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo, hatua ambayo mara kwa mara imekosolewa na wanaharakati katika nchi hiyo, ambao wanasema uhuru unatishiwa.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni © StateHouseUganda
Matangazo ya kibiashara

Kampala inasema imechukua hatua hii kwa sababu ina uwezo wa kuchunguza na kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa, hii ikiwa na maana kuwa ofisi hiyo haitaendelea kutoa huduma zake nchini humo muda wake ukikamilika mwaka huu.

Rekodi yetu ya haki za binadamu kwa miaka mingi imeimarika sana chini ya uongozi wa Rais (Yoweri) Museveni," amesema waziri wa Mambo ya Nje Henry Okello Oryem.

Oryem amesema Uganda, imezipa nguvu taasisi za ndani kama vile Shirika la kutetea haki za binadamu la Uganda na mashirika ya kiraia, ambayo yanasaidia yanafuatilia utendaji wake wa haki za binadamu.

Uamuzi huu wa serikali ya Uganda unakuja, wakati huu wanasiasa wa upinzani, wakiendelea kulalamikia ongezeko la visa vya ukikwaji wa haki za binadamu na wafuasi wao kukamatwa mara kwa mara na kuzuiwa, wanahabari kushambuliwa na wanasheria kufungwa jela.

Mnamo mwezi Novemba mwaka jana, kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya mateso, ilionyesha wasiwasi wake kuhusu ripoti kwamba mateso na unyanyasaji viliendelea kufanywa mara kwa mara nchini humo.

Ofisi ya haki za Umoja wa Mataifa jijini Kampala ilianzishwa mwaka 2005 na kibali chake cha kuhudumu nchini humo, kimekuwa kikifanywa upya kila baada ya miaka michache.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.