Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-UCHUMI

Tanzania yaidhinisha ujenzi wa bomba la mafuta lenye utata

Tanzania imeidinisha ujenzi wa bomba la mafuta lenye thamani ya dola bilioni 3.5 kama sehemu ya mradi mkubwa wenye utata wa kusafirisha hidrokaboni za Afrika Mashariki hadi katika masoko ya kimataifa, licha ya kukosolewa mara kwa mara na watetezi wa mazingira.

Kuidhinishwa kwa serikali ya Tanzania "kunaashiria hatua nyingine ya maendeleo kwa EACOP kwani itawezesha kuanza kwa shughuli kubwa za ujenzi nchini Tanzania, kufuatia mchakato wa upatikanaji wa ardhi unaoendelea", amesema Mkurugenzi Mkuu wa EACOP nchini Tanzania, Wendy Brown, kwenye mkutano wa kupokea cheti huko Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania.
Kuidhinishwa kwa serikali ya Tanzania "kunaashiria hatua nyingine ya maendeleo kwa EACOP kwani itawezesha kuanza kwa shughuli kubwa za ujenzi nchini Tanzania, kufuatia mchakato wa upatikanaji wa ardhi unaoendelea", amesema Mkurugenzi Mkuu wa EACOP nchini Tanzania, Wendy Brown, kwenye mkutano wa kupokea cheti huko Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania. Wikimédia/Muhammad Mahdi Karim
Matangazo ya kibiashara

Bomba hili lenye urefu wa takriban kilomita 1,500, litaunganisha visima vya Ziwa Albert, magharibi mwa Uganda, na pwani ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

Mradi huu unahitaji idhini ya nchi zote mbili na mwezi Januari, Uganda ilitoa leseni kwa muungano wa Kampuni ya East African Crude Oil Pipeline Company Ltd (EACOP), inayomilikiwa kwa 62% na kampuni kubwa ya Ufaransa ya TotalEnergies.

Kuidhinishwa kwa serikali ya Tanzania "kunaashiria hatua nyingine ya maendeleo kwa EACOP kwani itawezesha kuanza kwa shughuli kubwa za ujenzi nchini Tanzania, kufuatia mchakato wa upatikanaji wa ardhi unaoendelea", amesema Mkurugenzi Mkuu wa EACOP nchini Tanzania, Wendy Brown, kwenye mkutano wa kupokea cheti huko Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania.

Mradi huo "utazingatia sio tu sheria za Tanzania na Uganda, lakini pia viwango vikali vya kimataifa", hasa katika suala la "haki za binadamu", amesema Bi. Brown.

Mradi huo wenye thamani ya bilioni 10 kati ya Tanzania na Uganda, hata hivyo, umepata upinzani kutoka kwa wanaharakati wa mazingira na makundi yanayoamini kuwa unatishia mfumo wa ikolojia dhaifu wa eneo hilo na watu wanaoishi eneo hilo. Baadhi ya kaya 13,000 zimeathiriwa na njia ya bomba hilo, kulingana na Bi. Brown.

"Tunajivunia bomba hili kwa sababu litaongeza ushawishi wa Tanzania duniani," amesema January Makamba, Waziri wa Nishati wa Tanzania.

“Kuna kelele nyingi (dhidi ya) mradi huu, lakini tunaongeza juhudi za kuhifadhi mazingira”, ameongeza Bw. Makamba, akizungumzia mipango ya upandaji wa miti kwenye njia ya bomba. "Tumezingatia viwango vyote vya mazingira, usalama na haki za binadamu," pia amebainisha.

Mashirika sita yasiyo ya kiserikali yaliishtaki TotalEnergies mbele ya mahakama ya Paris mwishoni mwa 2022, na kulitaka kundi hilo kuheshimu sheria iliyopitishwa mwaka wa 2017 ambayo inalazimisha mashirika ya kimataifa "wajibu wa kuwa makini" kwa shughuli zao duniani. Majadiliano hayo yanatarajiwa tarehe 28 Februari.

Ziwa Albert, mpaka wa asili kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lina wastani wa mapipa bilioni 6.5 ya mafuta yasiyosafishwa, ambayo takriban bilioni 1.4 yanachukuliwa kuwa yanaweza kuokolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.