Pata taarifa kuu

Lourenço aliwasiliana na M23 baada mkutano wa AU

NAIROBI – Rais wa Angola João Lourenço ambaye pia ni Mwenyekiti wa kongamano la Kimataifa la Eneo la Maziwa Makuu (ICGLR), amesema kulikuwa na mawasiliano na uongozi wa waasi wa M 23 lakini hayajazaa matunda.

Rais wa Angola João Lourenço na mwenzake Félix Tshisekedi DRC
Rais wa Angola João Lourenço na mwenzake Félix Tshisekedi DRC © Facebook Presidência de Angola
Matangazo ya kibiashara

Jitihada hizi zilikuja baada ya mkutano wa wakuu wa nchgi za Afrika jijini Addis Ababa katikati ya mwezi Februari.

Serikali ya Kinshasa imezungumzia hatua hii, kama anavyoleza msemaji wake Patrick Muyaya.

“ilikuwa ni kuepusha kulegalega kwa mambo kama tulivyoshuhudia kule nyuma iliwasiseme hatukuwa tunafahamu na ndicho rais Lorenco alichokifanya.”amesema Patrick Muyaya

Kwa mujibu wa mkutano uliofanyika jijini Nairobi na Luanda, ilikubaliwa kuwa waasi wa M23 wataondoka katika maeneo wanayokaliwa swala ambalo baadhi ya wakazi katika sehemu hizo mashariki ya DRC wamesema suala hilo halijaafikiwa.

Licha ya hayo wanajeshi wa serikali ya DRC kwa ushirikiano na wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wameendelea kukabiliana na makundi ya waasi yakiwemo M23 na ADF, waasi hao wakituhumiwa kwa kuwashambulia raia wa mashariki ya DRC.

Kwa upande mwengine, Marekani imetangaza itatoa zawadi ya hadi dola milioni tano,kwa yeyote atakayetoa taarifa kusaidia kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la waasi la ADF Seka Musa Baluku,ambaye ana asili ya Uganda.

Mwaka 2021, Marekani iliorodhesha kundi la ADF katika orodha ya makundi ya kigaidi,ikihusishwa na kundi la Islamic state. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.