Pata taarifa kuu

Angola: Bunge kujadili hatua ya kutumwa kwa wanajeshi wake DRC

NAIROBI – Bunge la Angola siku ya Ijumaa, litathathmini ombi la kutumwa kwa jeshi lake Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya tangazo la rais Joao Lourenco, ambaye ni msuluhishi wa mzozo unaoendelea kutoka nchi za Maziwa Makuu.

Bunge nchini Angola wiki linatarajiwa kujadili hatua ya kutumwa kwa wanajeshi wake mashariki ya DRC
Bunge nchini Angola wiki linatarajiwa kujadili hatua ya kutumwa kwa wanajeshi wake mashariki ya DRC © Catarina Falcao
Matangazo ya kibiashara

Serikali jijini Kinshasa inasema kikosi cha Angola hakiji kupigana bali kuhakikisha kuwa makubaliano ya Luanda, yaliyotaka waasi wa M 23 na makundi mengine yanaacha vita na kuondoka katika maeneo wanayodhibiti, yanaheshimiwa na kutekelezwa.

Jumamosi iliyopita, wakati alipotangaza hatua hiyo, raia wa Angola, alisisitiza kuwa wanajeshi wake watakuja kuhakikisha kuwa raia wanakuwa salama, na kuondoka kwa waasi wa M 23 katika maeneo ambayo wanadhibiti.

Aidha, kikosi hicho kitakuja kuchunguza madai ya DRC kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi wa M 23, suala ambalo limeharibu uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

Hata hivyo, mpaka sasa haijafahamika idadi ya wanajeshi wa Angola watakaotumwa Mashariki mwa DRC na muda watakaokuwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.