Pata taarifa kuu

Uganda kuwatuma wanajeshi Elfu Moja Mashariki mwa DRC

NAIROBI – Uganda inatarajiwa kutuma wanajeshi wake Elfu 1, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwezi huu kuungana na kikosi cha ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wanajeshi wa Uganda kutumwa nchini DRC katika eneo la mashariki kupambana na waasi wa M23 wanaoendelea kuwahangaisha raia
Wanajeshi wa Uganda kutumwa nchini DRC katika eneo la mashariki kupambana na waasi wa M23 wanaoendelea kuwahangaisha raia AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Hili limethibitihswa na Kanali Mike Walaka Hyeroba, ambaye amesema vikosi hivyo vya Uganda vitatumwa katika jimbo la Kivu Kaskazini ambalo limekuwa likishuhudia mapigano kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali, FARDC.

Kikosi cha Uganda, kitajiunga na vile vya Kenya na Burundi, ambavyo vimekuwa Mashariki mwa DRC kwa miezi kadhaa sasa. Licha ya uwepo wao, vita vimeendelea kushuhudiwa na kuzua hasira miongon mwa raia wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia DRC, mwaka uliopita, vikosi hivyo viliingia nchini na kuungana na vile vya FARDC kupambana na waasi wa ADF, lakini licha ya muungano huo, mauaji ya raia yameendelea kushuhudiwa.

Waasi wa M 23 ambao siku kadhaa walitangaza kujiondoa katika baadhi ya maeneo waliyoshikilia, wamechukua maeneo mengi ya Kivu Kaskazini, hali inayoendelea kuzua hali ya wasiwasi Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.