Pata taarifa kuu

Uganda: Waziri Gorette na kaka yake wanazuiliwa kwa kashfa ya ufisadi

NAIROBI – Mahakama inayoshughulikia kesi za ufisadi nchini Uganda, Alhamis ya wiki hii iliagiza kuendelea kuzuiliwa kwa waziri wa Serikali na kaka yake kwa tuhuma za kutumia vibaya mali ya uma, katika moja ya kesi ya rushwa inayomuhusisha afisa wa juu katika Serikali.

Polisi nchini Uganda wanamzuilia waziri  Mary Gorette Kitutu na Kaka yake kwa tuhumua za ufisadi

vibaya mali ya uma
Polisi nchini Uganda wanamzuilia waziri Mary Gorette Kitutu na Kaka yake kwa tuhumua za ufisadi vibaya mali ya uma Reuters/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo Mary Gorette Kitutu na Kaka yake, walifikishwa mahakamani hapo jana wakituhumiwa kuiba mabati yaliyokuwa yatumike kuzisaidia familia masikini katika eneo la Karamoja.

Watuhumiwa wote wawili walishtakiwa kwa makosa mawili, kuisababishia hasara serikali na kupanga njama za udanganyifu.

Kwa mujibu wa mawakili wao, Mary kaka yake wamerudishwa rumande wakisubiri kurejeshwa tena mahakamani April 12.

Kashfa hii ya mabato ambayo inawahusisha maofisa wengine wajuu kwenye Serikali, ilizua mjadala mkubwa nchini humo na hasa kupitia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ambapo raia wamekashifu Serikali kufumbia macho vitendo vya rushwa.

Tukio la mwisho kwa afisa wa juu serikali kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa lilikuwa ji la mwaka 2007, ambapo waliokuwa mawaziri Jim Muhwewi  na Mike Mukula , walishtakiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za misaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.