Pata taarifa kuu

Waziri wa fedha nchini Uganda amekamatwa akihusishwa na wizi wa mabati

NAIROBI – Waziri wa fedha nchini Uganda Amos Lugoloobi amekamatwa akihusishwa na wizi wa mabati yaliyonunuliwa na serikali kuwasaidia watu masikini katika eneo la Karamoja, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi (Mipango), Jamhuri ya Uganda
Waziri wa Nchi anayeshughulikia Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi (Mipango), Jamhuri ya Uganda © Uganda ministry of Finance
Matangazo ya kibiashara

Lugoloobi, anakuwa Waziri wa pili kukamatwa baada ya Mary Goretti Kitutu, anayehusika na masuala ya Karamoja, kutiwa mbarano wiki moja iliyopita, na kufunguliwa mashtaka.

Fred Enanga, msemaji wa polisi amethibitisha kukamatwa kwa Waziri huyo ambaye sasa atafunguliwa mashtaka Mahakamani akihusishwa na kosa la wizi wa mali ya umma.

Kwa mujibu wa polisi, kuna Mawaziri 10, wabunge 31 na maafisa 13 wa serikali, wanaochunguzwa kuhusiana na wizi wa mabati hayo yaliyolenga kuwajengea watu masikini nyumba zenye bei nafuu.

Tukio la kukamatwa kwa Mawaziri wanaohusishwa na madai ya ufisadi, sio jambo la kawaida nchini Uganda. Kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi anaishtumu serikali ya rais Yoweri Museveni kwa kutofanya vya kutosha kukabiliana na rushwa, akiishtumu kwa kufuja Mabilioni ya Dola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.