Pata taarifa kuu

Uganda yajiandaa kuondoa kwa awamu majeshi yake nchini Somalia

NAIROBI – Mawaziri wa ulinzi na Mambo ya nje kutoka nchi zilizo na vikosi vyake nchini Somalia, wamekutana jijini Kampala, kujadili utaratibu wa kuanza kuondoka kwa wanajeshi hao, na kutathmini hali ya usalama katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Uganda wanaounda jeshi la AMISOM nchini Somalia
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Uganda wanaounda jeshi la AMISOM nchini Somalia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo uliwakutanisha pia wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Wadau walioshiriki kwenye mkutano huo, wamesema kuwepo kwa kikosi hicho cha ATMIS chini ya Umoja wa Afrika, kimesaidia kuanza kuimarika kwa usalama na kufikia Juni 30 mwaka huu, kundi la kwanza la wanajeshi Elfu mbili wataanza kuondoka. 

 Abubakhar Jeje Odongo, ni Waziri wa Mambo ya nje wa Uganda. 

Kwa hivyo ni busara kufanya tathmini ya pamoja ya hali ya usalama, kupanga na kuratibu kutekeleza ratiba za kuchora na kwa Serikali ya Shirikisho la Somalia kuhakikisha uzalishaji wa nguvu na ujumuishaji kuchukua majukumu ya usalama, amesema Odongo.
00:28

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda, Jeje Odongo

Hata hivyo, Umoja wa  Mataifa kupitia mmoja wa wawakilishi wake nchini Somalia, Aisa Kirabo Kacyira anasema nchi hiyo bado inahitaji msaada zaidi ili kuimarisha usalama wake wakati kikosi cha ATMIS kitakapoondoka. 

Tungependa pia kupendekeza kuongezeka kwa usaidizi katika ukuzaji wa uwezo wa vifaa wa Somalia ambao ni wa kutosha, wa bei nafuu na endelevu. Hii itahusisha, miongoni mwa mambo mengine, uwezo wa ziada na wa hali ya juu kwa Vikosi vya Usalama vya Somalia katika nyanja mbalimbali za usafirishaji, amesema Aisa.
00:29

Aisa Kirabo, mmoja wa wawakilishi wa UN nchini Somalia

Kikosi kinachoundwa na mataifa ya Burundi, Djibouti, Ethiopia Kenya na Uganda, kinatarajiwa kumaliza operesheni zake dhidi ya Al Shabab kufikia mwisho wa mwaka ujao. 

 

Ripoti ya Kenneth Lukwago, mwandishi wa RFI Kiswahili, jijini Kampala

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.