Pata taarifa kuu

Waziri wa leba wa Uganda auawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake

NAIROBI – Waziri wa Leba, Ajira na Mahusiano ya Viwanda, nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola, ameuawa Jumanne asubuhi kwa kupigwa risasi na mlinzi wake.

Aliyekuwa waziri wa Leba nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola
Aliyekuwa waziri wa Leba nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola © Parliament of the Republic of Uganda
Matangazo ya kibiashara

Kanali Engola ameuawa nyumbani kwake Kyanja, kiungani mwa jiji la Kampala, na mlinzi wake ambaye pia dakika chache baadaye alijiua kwa kujipiga risasi.

Baadhi ya walioshuhudia tukio hili wansema, mlinzi huyo alizunguka katika eneo hilo akifyatua risasi hewani, ripoti zikisema kuwa baadhi ya watu walijeruhiwa katika tukio hilo.

Naibu msemaji wa polisi wa Kampala Metropolitan, Luke Owoyesigire, amethibitisha kisa hiki kwenye njia ya simu na shirika la habari la Daily Monitor.

Ndio, ukienda Kyanja kuna ufyatuliaji risasi ambao umetokea. Mlinzi amemuua muajiri wake, amesema Owoyesigire.

Spika wa bunge la Uganda, Anita Among, pia amethibitisha tukio hili wakati akiendesha kikao cha bunge Jumanne asubuhi.

Asubuhi hii nimepokea taarifa za kusikitisha kuwa mheshimiwa Engola ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake, ambaye pia amejiua, Amesema Among.

Mmoja wa walioshuhudia tukio, amesema mlinzi huyo hakuwa amelipwa mshahara wake.

Mlinzi alisema kuwa hakuwa amelipwa. Alisema ana mke ambaye ni mjamzito and watoto wake hawakuwa wanaenda shuleni wakati wa muajiri wake walikuwa wanaenda, alisema mmoja wa mashuhuda.

Waziri Engola aliwahi kuhudumu kama naibu waziri wa ulinzi wa Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.