Pata taarifa kuu

Kenya na Uganda kutafuta mfadhili mbadala kwa ajili ya mradi wa reli ya kisasa

NAIROBI – Kenya na Uganda, sasa zitalazimika kutafuta mfadhili mbadala kwa ajili ya mradi wa reli ya kisasa itakayounganisha mji wa Naivasha na Kampala kupitia malaba, wamenukuliwa maofisa wa serikali zote mbili.

Reli ya kisasa ilitarajiwa kurahisisha uchukuzi kati ya nchi jirani za Kenya na Uganda
Reli ya kisasa ilitarajiwa kurahisisha uchukuzi kati ya nchi jirani za Kenya na Uganda AP - Khalil Senosi
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti moja la ukanda The East African, afisa mmoja katika wizara ya ujenzi nchini Uganda, amethibitisha nchi zao kutafuta mfadhili kutoka nchi za Ulaya bila hata hivyo kuitaja nchi yenyewe.

Hatua hii inamaanisha kuwa maendeleo ya mradi wa reli ya kilometa 273 ambayo ujenzi Wake ulisimama kwa muda, sasa utafufuliwa na itatokea jijini Kampala Uganda hadi kwenye mji wa Mombasa nchini kenya.

Wakati Uganda ikijaribu kutafuta wafadhili zaidi, Kenya kwa upande wake imesema tayari ina deni kubwa la kulipa kwa nchi ya China na kwamba haina mpango wa kukopa zaidi kutoka kwa taifa hilo licha ya ukweli kuwa wamekuwa kwenye mazungumzo kuangalia uwezekano wa kupata mkopo wenye masharti nafuu.

Haya yanajiri baada ya juma lililopita, Uganda kudai kuwa ujenzi wa reli hiyo utakao gharibu dola za Marekani Bilioni 2.2 utaanza tena mwaka huu, baada ya mazungumzo yake na Serikali ya china kuhusu kupewa mkopo kugonga mwamba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.