Pata taarifa kuu

DRC : Maofisa wa usalama wafanya msako katika makazi ya Katumbi

NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa usalama wamefanya msako jijini Kinshasa na Lubumbashi katika makaazi ya mwanasiasa wa upinzani Moïse Katumbi na mshauri wake wa kisiasa Salomon Kalonda, aliyekamatwa wiki iliyopita. Chama cha Katumbi kinasema hatua hii ni mwendelezo wa kumhangaisha mgombea wake asiwanie urais. 

Moïse Katumbi, Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC
Moïse Katumbi, Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Msako wa makazi ya Salomon Kalonda huko Lubumbashi siku ya Alhamis ulifanyika kwa saa tano kuaanzia saa tatu asubuhi.

Barabara katika êneo hilo zilizingirwa na askari jeshi. Hata hivyo, familia ya Salomon na wanasheria wake walizuiwa na maofisa wa polisi kuingia katika êneo hilo. 

Kwake Hubert Tshwaka, mtetezi wa haki za binadamu aliyefuatilia msako huo amesema kulikuwa na ukiukaji wa utaratibu na kueleza kuwa oparesheni Ilifanyika bila ya kuwepo kwa mashahidi.

Wakati huo huo mjini Kinshasa, makazi ya Moïse Katumbi nayo pia yalitembelewa na wanajeshi. Hapo pia, msako ulifanyika kinyume na sheria za nchi kama alivyoeleza katibu wa Chama Cha upinzani Ensemble pour la République

Katika taarifa iliyotolewa mjini Kinshasa Alhamisi jioni, Dieudonné Bolengetenge ameikosoa mamlaka ya Kinshasa dhidi ya kuendeleza oparesheni hizo dhidi ya Moïse Katumbi, aliyetangazwa kuwa mgombea urais Desemba ijayo. 

Kwa sasa, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu matokeo ya msako huu. Bali Hubert Tshiswaka, mtetezi wa Haki za binadamu   umaanisha kua wanajeshi walichukua sefu ama sanduku na vifaa vigine kutoka kwa makazi ya Salomon.

Taarifa ya Mwandishi wetu wa Lubumbashi Denise Maheho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.