Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Ufaransa yalaani 'shambulio la kikatili' nchini Uganda

Ufaransa inalaani "vikali shambulio la kikatili" dhidi ya shule ya upili magharibi mwa Uganda, ambalo limesababisha vifo na majeruhi kadhaa, kulingana na taarifa ya Jumamosi na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Uganda: mvulana huyu anafarijiwa baada ya shambulio lililohusishwa na ADF kwenye shule ya upili ya Lhubiriha, huko Mpondwe, karibu na Bwera magharibi mwa nchi.
Uganda: mvulana huyu anafarijiwa baada ya shambulio lililohusishwa na ADF kwenye shule ya upili ya Lhubiriha, huko Mpondwe, karibu na Bwera magharibi mwa nchi. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu 41 wameuawa, wengi wao wakiwa wanafunzi, katika uvamizi uliofanywa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi Juni 17 na wanajihadi dhidi ya shule, shambulio baya zaidi la aina hii kuwahi kutokea nchini Uganda kwa miaka mingi.

Maafisa wa jeshi na polisi wamewalaumu wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF), wanamgambo wa Kiislamu ambao walitangaza kuwa sehemu ya kundi la Islamic State, baada ya shambulio la umwagaji damu katika shule ya sekondari wilayani Kasese, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

"Ufaransa inatuma rambirambi zake kwa familia na ndugu, jamaa na marafiki wa wahanga, kwa mamlaka ya Uganda na kuelezea mshikamano wake na waliojeruhiwa," ameongeza msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.