Pata taarifa kuu

Papa Francis ameongoza maombi kwa ajili ya waathiriwa wa shambulio nchini Uganda

NAIROBI – Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameongoza maombi mjini Vatican kwa ajili ya waathiriwa wa shambulio la kigaidi kwenye shule mmoja nchini Uganda.

Baadhi ya familia zimeanza kuwazika wapendwa wao
Baadhi ya familia zimeanza kuwazika wapendwa wao AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

Karibia watu 40-wengi wao wakiwa ni wanafunzi, waliripotiwa kuawaua kwa kukatwa kwa mapanga, kupigwa risasi na kuchomwa moto katika mji wa Magharibi wa  Mpondwe  Ijuma usiku.

Jeshi la Uganda limesema kuwa linawasaka waasi wa kundi la ADF wanaotuhumiwa kwa kutekeleza shambulio hilo ambalo limekashifiwa vikali kote duniani.

Kando na kutekeleza mauaji hayo, waasi hao wanaoendeleza shughuli zao mashariki mwa DRC, wametuhumiwa kwa kuwateka wanafunzi sita kabla ya kuvuka mpaka na kuingia nchini DR Congo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amelaani shambulio hilo ambalo amelitaja kuwa la kioga.

Baadhi ya familia zimeanza kuchukua miili ya wapendwa wao kwa ajili ya mazishi
Baadhi ya familia zimeanza kuchukua miili ya wapendwa wao kwa ajili ya mazishi AP - Hajarah Nalwadda

Kwa mujibu wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ameagiza kutumwa kwa wanajeshi zaidi katika mpaka wa nchi hiyo na DRC, baada ya shambulio la hilo.

Aidha katika taarifa yake, rais Museven, amehoji ilikuwaje jeshi lake lililoko nchini DRC lilishindwa kubaini mtego wa kundi hilo. Matamshi yake yalifuatia yale yaliyotolewa na mke wake Janet Museveni.

Tayari jeshi limesema linawashikilia watu kadhaa kwa mahojiano, wakati huu wakijaribu kubaini ni watu wangapi waliotekwa nyara na kundi hilo ingawa idadi ya awali ni watu 6 wakati huu baadhi ya familia zikianza kuwachukua wapendwa wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.