Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa: Waasi wa ADF wanafadhiliwa na kundi la Islamic State

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamebaini kuwa waasi wa ADF, wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC na kulaumiwa kwa shambulio la Ijumaa kwenye shule moja nchini Uganda, wanapata msaada wa kifedha kutoka kwa kundi la Islamic State na kutaka kupanua eneo lao la operesheni, kulingana na ripoti wataalamu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumatatu.

Familia zilizoomboleza katika mazishi ya Florence Masika na Zakayo Masereka huko Mpondwe Jumapili, Juni 18, 2023. Florence na Zakayo waliuawa na washambuliaji wanaoaminika na mamlaka kuwa ni kutoka kwa wanamgambo wa ADF wenye makao yake DRC. Watu 41, wengi wao wakiwa wanafunzi, waliuawa katika shambulizi ambalo ni baya zaidi nchini Uganda tangu 2010. Wahanga walipigwa risasi au kuchomwa moto hadi kufa katika uvamizi wa usiku wa kuamkia siku ya Jumapili katika Shule ya Sekondari ya Lhubiriha huko Mpondwe, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Familia zilizoomboleza katika mazishi ya Florence Masika na Zakayo Masereka huko Mpondwe Jumapili, Juni 18, 2023. Florence na Zakayo waliuawa na washambuliaji wanaoaminika na mamlaka kuwa ni kutoka kwa wanamgambo wa ADF wenye makao yake DRC. Watu 41, wengi wao wakiwa wanafunzi, waliuawa katika shambulizi ambalo ni baya zaidi nchini Uganda tangu 2010. Wahanga walipigwa risasi au kuchomwa moto hadi kufa katika uvamizi wa usiku wa kuamkia siku ya Jumapili katika Shule ya Sekondari ya Lhubiriha huko Mpondwe, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. AFP - STUART TIBAWESWA
Matangazo ya kibiashara

Moja ya makundi mengi yenye silaha yanayozunguka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ADF (Allied Democratic Forces) ni miongoni mwa makundi mabaya zaidi, yanayoshutumiwa kuua maelfu ya raia huko.

Waasi wa Kiislamu wa Uganda, walioanzishwa nchini DRC tangu miaka ya 1990, waliahidi kujiunga na kundi la IS mwaka 2019, ambalo linadai baadhi ya vitendo vyao na kuvionyesha kama "jimbo lake la Afrika ya Kati" (Iscap kwa Kiingereza).

Lakini ufadhili wao na IS hadi sasa haujaandikwa.

Katika ripoti yake ya hivi punde, inayotarajiwa kutolewa wiki hii, kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC linasema IS "imetoa msaada wa kifedha kwa ADF tangu mwaka 2019, kupitia mfumo tata wa kifedha unaohusisha watu binafsi katika nchi kadhaa za bara, zinazotoka Somalia na kupitia Afrika Kusini, Kenya na Uganda".

Wataalamu hao pia wanaonyesha kuwa ADF "ilituma wapiganaji na/au washirika katika misheni ya upelelezi kujaribu kupanua eneo lao la operesheni mbali na mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri". Kulingana na kundi hili, "walitaka kusajili na kufanya mashambulizi mjini Kinshasa" na pia katika mikoa ya Tshopo, Haut-Uélé (kaskazini mashariki) na Kivu Kusini, mashariki mwa DRC.

Maafisa wa Uganda wanashutumu ADF kwa kufanya shambulio katika shule ya upili nchini Uganda, karibu na mpaka wa DRC, ambalo lliua takriban watu 41 usiku wa Ijumaa kuamkiaJumamosi.

Uganda na DRC zilianzisha mashambulizi ya pamoja mwaka 2021 ili kuwatimuwa ADF kutoka ngome zao nchini DRC, hadi sasa zimeshindwa kukomesha mashambulizi ya kundi hilo.

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa pia wanatoa sehemu kubwa ya utafiti wao usaidizi wa Rwanda kwa waasi wa M23 huko Kivu Kaskazini, madai ambayo walikuwa wameyaweka katika ripoti za awali, ingawa Kigali inakanusha.

Wanabainisha kuwa "wamepata ushahidi mwingine wa uingiliaji kati wa moja kwa moja wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) katika ardhi a DRC" na "kutambua makamanda na maafisa kadhaa wa RDF wanaoratibu operesheni za RDF nchini DRC".

Kwa ujumla, wanaona kuwa "hali ya usalama na kibinadamu katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini imeendelea kuzorota kwa kiasi kikubwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.