Pata taarifa kuu

Uganda ni salama licha ya tahadhari za kiusalama: Polisi

Nairobi – Vyombo vya usalama nchini Uganda, vinasema taifa hilo liko salama, licha ya tahadhari mpya kuhusu uwezekano wa kutekelezwa shambulio la kigaidi, iliyotolewa na ubalozi wa Uingereza nchini humo.

Msemaji wa polisi nchini Uganda
Msemaji wa polisi nchini Uganda © Uganda police
Matangazo ya kibiashara

Katika tarifa kwa raia Wake, serikali ya Uingereza imesema kupitia taarifa za kiintelijensia walizokusanya, kuna uwezekano mkubwa magaidi wakatekeleza mashambulio nchini Uganda.

Aidha tarifa hiyo imeongeza kuwa mashambulio yanayoshukiwa kutekelezwa hayatakuwa kwa mpango, kuwalenga raia wa kigeni au maeneo ambayo wanapenda kutembelea.

Jijini Kampala, happ jana msemaji wa jeshi Biregdia Felix Kulayigye, amesema tishi la ukaidi linaweza kutekelezwa kwenye nchi yoyote ikiwemo Uingereza na kwamba watailinda nchi yao.

Kwa upande Wake msemaji wa polisi, Fred Enanga, aliwahakikishia raia kuhusu usalama wao na kuongeza kuwa jeshi limejipanga kwa kushirikiana na idara nyingine za usalama, kuhakikisha wanadhibiti tukio lolote la uhalifu au ugaidi.

Onyo la Uingereza limekuja siku chache kupita tangu mwezi uliopita, wanajihadi wa ADF watekeleze shambulio katika shule moja mjini Kasese na kuuwa watu zaudu ya 40 wakiwemo wanafunzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.