Pata taarifa kuu

DRC: Mlinzi Cherubin Okende ahojiwa na polisi

Mlinzi wa mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo aliyeuawa kwa kupigwa risasi wiki iliyopita mjini Kinshasa anahojiwa na polisi.

Cherubin Okende, alikuwa mshirika wa karibu wa Moise Katumbi
Cherubin Okende, alikuwa mshirika wa karibu wa Moise Katumbi AP - Samy Ntumba Shambuyi
Matangazo ya kibiashara

Aliyekuwa waziri wa uchukuzi, Cherubin Okende, alipatikana amefariki ndani ya gari lake baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Mwanasheria mkuu Firmin Mvonde amewambia wanahabari kwamba risasi iliyomuua mwanasiasa huyo, ilifyatuliwa kutoka ndani ya gari, silaha ikiripotiwa kupatikana karibu na Okende.

Alikuwa msemaji wa chama cha upinzani kinachoongozwa na Moïse Katumbi, ambaye anatarajiwa kugombea uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki jijini Kinshasa, Kadinali Fridolin Ambongo, hapo jana amesisitiza kauli yake ya awali kuwa mauaji ya mwanasiasa Cherubin Okende, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Moise Katumbi, yalipangwa.

Kadinali Ambongo amesema haya wakati wa misa maalumu kumkumbuka Okende ambaye aliwahi pia kuwa waziri wa Usafiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.