Pata taarifa kuu

Uganda: Watu 20 wafariki katika ajali ya boti

Watu 20 wamethibitishwa kufariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama maji kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda, ajali iliyotokea maajira ya saa tano asubuhi ya leo.

Boti la uvuvi kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda.
Boti la uvuvi kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda. Damiano Luchetti/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo ilikuwa na watu 34 na ilikuwa ikitokea kisiwa cha Bukasa kuelekea Entebbe, ambapo polisi wanasema watu 9 wameokolewa, huku chanzo cha ajali hiyo kimethibitishwa kuwa ni upakiaji kupita kiasi na hali mbaya ya hewa

Kwa mujibu wa maofisa wa polisi nchini humo, boti hiyo ambayo ilikuwa imejaa kupita kiasi, ilikuwa pia imebeba magunia ya makaa, chakula na bidhaa nyengine.

Polisi wanasema ajali hiyo ilisababisha na hatua ya wahudumu wa boti hiyo kujaza watu na mizigo kupita kiasi, hali mbaya ya anga pia ikitajwa kuwa chanzo na kuzama kwa chombo hicho.

Maofisa wa uokoaji wakiwemo polisi na wanaheshi walikuwa wakiendelea na shughuli za kujaribu kuwatafuta watu waliotoweka. Ajali za boti sio kawaida nchini Uganda.

Mwaka wa 2020, karibia watu 26 walifairiki katika Ziwa Albert kwenye mpaka wa Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Miaka miwili kabla, watu wengine walithibitishwa kufariki baada ya boti iliyokuwa imewabeba karibia watu 100 kuzama kwenye Ziwa Victoria karibu na jiji kuu la Kampala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.