Pata taarifa kuu

UN kufunga afisi zake kuhusu haki za binadamu nchini Uganda

Nairobi – Umoja wa mataifa unasema unafunga afisi zake kuhusu haki za binadamu nchini Uganda baada ya kuhudumu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kwa kipindi cha karibia muongo mmoja.

Umoja wa mataifa unasema umeafikia uamuzi huo baada ya serikali ya Kampala kukataa kuongeza muda wake wa kuhudumu
Umoja wa mataifa unasema umeafikia uamuzi huo baada ya serikali ya Kampala kukataa kuongeza muda wake wa kuhudumu AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa mataifa unasema umeafikia uamuzi huo baada ya serikali ya Kampala kukataa kuongeza muda wake wa kuhudumu kama iliyotakiwa.

Katika taarifa yake, UN imesema tayari afisi zake ndogo katika maeneo ya Gulu na Moroto zimefungwa kuelekea kutamatishwa rasimi kwa shughuli zake wikendi hii.

Mkuu wa haki za binadamu katika umoja huo Volker Turk ameeleza kwamba tangu kufunguliwa rasimi kwa afisi zao jijini Kampala mwaka wa 2005, wamefanikiwa kutatua masuala kadhaa yanayohusiana na haki za raia wa Uganda.

UN imesema tayari afisi zake ndogo katika maeneo ya Gulu na Moroto zimefungwa kuelekea kutamatishwa rasimi kwa shughuli zake wikendi hii
UN imesema tayari afisi zake ndogo katika maeneo ya Gulu na Moroto zimefungwa kuelekea kutamatishwa rasimi kwa shughuli zake wikendi hii © AFP - MUNIR UZ ZAMAN

Turk aidha ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya haki za binadamu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2026 wakati ikielezwa kwamba watetezi wa haki, mashirika ya kiraia na wanahabari wanakabiliwa na changamoto katika kuendeleza harakati zao.

UN pia imekosoa kile ambacho imetaja ni kuendelea kudorora kwa uhuru wa kujieleza, ikirejelea mashirika kadhaa ya kiraia ambayo mamlaka ya Uganda imesitisha shughuli zake katika kipindi cha miaka mwili iliyopita.

Umoja wa mataifa vilevile umekashifu sheria ambayo imepitishwa hivi majuzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, ikisema ni ya kibaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.