Pata taarifa kuu

Wanamaji 5 wa jeshi la Uganda walinusurika kifo baada ya boti yao kuzama

Nairobi – Maafisa watano wa jeshi la wanamaji la Uganda waliokuwa katika harakati ya kuopoa miili ya watu waliozama katika  ajali iliyotokea wiki iliyopita katika Ziwa Victoria wameokolewa hapo jana Jumapili baada ya mashua yao ya uokoaji kupinduka, polisi katika taifa hilo la Afrika Mashariki wamethibitisha.

Zoezi la kutafuta miili ya watu 15 waliozama katika ajali nyingine ya boti Agosti 2 ambapo watu 20 walipoteza maisha katika ziwa Viktoria linaendelea
Zoezi la kutafuta miili ya watu 15 waliozama katika ajali nyingine ya boti Agosti 2 ambapo watu 20 walipoteza maisha katika ziwa Viktoria linaendelea Damiano Luchetti/wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu 20 walifariki katika ajali hiyo Jumanne iliyopita iliyohusisha boti iliyokuwa imejazwa  mizigo ikidaiwa kuwa raia 34 walikuwa wameabiri chombo hicho. Watu tisa waliokolewa huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Siku ya Jumamosi, polisi walisema walikuwa wameopoa miili mitano tu, yote ikwia ni ya wanawake, maofisa nchini humo wakisema wanakabiliwa na changamoto kutokana na hali mbaya ya hewa kwenye  ziwa hilo kutokana na mvua kubwa inayoendelea.

Licha ya hayo, maofisa wa polisi wanasema  uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa baada ya shughuli hiyo kukamilika wakati huu pia utafutaji wa miili ya watu waliozama  ikiwa bado inaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.