Pata taarifa kuu

Uganda: Kijana wa miaka 20 aliyeshtakiwa kwa "ushoga uliokithiri" akabiliwa na hukumu ya kifo

Hukumu hii imewezekana tangu kuanza kutumika kwa sheria mpya mwezi Mei mwaka huu, mojawapo ya adhabu kali zaidi duniani kulingana na waangalizi kadhaa wa kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa mtu kufunguliwa mashitaka kwa sababu hii.

Kwa upande wake, wakili wa mshtakiwa anabaini kuwa sheria iliyotangazwa mwezi Mei ni kinyume cha katiba.
Kwa upande wake, wakili wa mshtakiwa anabaini kuwa sheria iliyotangazwa mwezi Mei ni kinyume cha katiba. DR
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na msemaji wa upande wa mashtaka wa Uganda, kijana huyo alishtakiwa huko Soroti, jiji lililo katikati-mashariki mwa nchi hiyo na kuwekwa kizuizini kabla ya kusikilizwa kwa kesi, mnamo Agosti 18.

Hati ya mashtaka ambayo mashirika ya habari ya AFP na Reuters inataja "kujihusisha na mapenzi yaliyokithiri ya jinsia moja na mwanamume mtu mzima mwenye umri wa miaka 41". Lakini bila kubainisha kwa nini sifa ya "ushoga uliokithiri" imehifadhiwa. Hata hivyo, kulingana na habari yetu, mmoja wa wanaume wawili waliohusishwa ni mlemavu, na kwa hivyo anachukuliwa kuwa mtu dhaifu. Kwa vyombo vya shria vya Uganda, kwa vyovyote vile ni mara ya kwanza kwa mtu kushtakiwa kwa sababu hii nchini humo.

Kwa upande wake, wakili wa mshtakiwa anabaini kuwa sheria iliyotangazwa mwezi Mei ni kinyume cha katiba. Lakini ikiwa nakala hii ilipingwa mbele ya mahakama, hakuna chombo ambacho bado kimechukua kesi hiyo ... Ambayo ina maana kwamba sheria inaweza kutumika na majaji na hukumu ya kifo kutamkwa.

"Kwa hivyo nina wasiwasi na jamii yangu"

Frank Mugisha ni mmoja wa wanaharakati pekee wa LGBT nchini. Anatumai kubatilisha sheria lakini hafichi hofu yake baada ya kufunguliwa mashtaka: “Hatua yangu ya kwanza ilikuwa hofu. Kwa sababu najua kuwa mara tu habari za aina hii zinapochapishwa kwenye vyombo vya habari, kuna athari karibu kila wakati. Mashirika ya serikali lakini pia watu pia hushambulia watu wa jamii ya LGBT. Kwa hivyo nina wasiwasi kuhusu jumuiya yangu kwa sababu huenda itawapata wengine hivi karibuni. Sheria hii inatumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi na kujiongezea umaarufu nchini Uganda. Haina sababu ya kuwepo na hakuna kinachoweza kuihalalisha kwa sababu watu wanaojihussha na mapenzi ya jinsi mmoja hawana madhara! Kwa kweli, sheria hii haimlindi mtu yeyote, mbaya zaidi: inahatarisha jamii ya LGBTQ. Na nina hakika kwamba wakati fulani mamlaka itatambua kwamba nakala hii sio mazuri kwa nchi. Na kwamba itafutwa. "

Kutokana na majadiliano Bungeni, muswada huo uliamsha hasira za jumuiya ya kimataifa na watetezi wa haki za binadamu. Na kama Uganda haijamnyonga mtu yeyote kwa miaka ishirini, hukumu ya kifo bado inatumika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.