Pata taarifa kuu

Uganda: Mahakama kuanza kusikiliza kesi ya kupinga sheria dhidi ya ushoga

Nairobi – Mahakama ya kikatiba nchini Uganda inatazamiwa  kuanza kusikiliza malalamishi matatu ya kupinga sheria dhidi ya ushoga iliyoanza kutumika kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki mwezi Mei.

Sheria hiyo  inatoa adhabu ya kifo kwa wale wanaopatikana na hatia ya kujihusisha vitendo vya jinsia moja
Sheria hiyo  inatoa adhabu ya kifo kwa wale wanaopatikana na hatia ya kujihusisha vitendo vya jinsia moja REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo  inatoa adhabu ya kifo kwa wale wanaopatikana na hatia ya kujihusisha vitendo vya jinsia moja ikiwa ni pamoja na adhabu ya kifo kwa kile kinachotajwa kama"ushoga uliokithiri" , hatia ambayo inaweza kuhusisha ngono na watoto au watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa na kundi la watu binafsi na mashirika ya haki za binadamu, sheria hiyo ilipitishwa bila ushiriki wa kutosha kutoka kwa  umma na pia inakiuka baadhi ya haki na uhuru wa kikatiba.

Aidha walalamishi wanasema kuwa kamati ya masuala ya sheria na bunge ilichukua muda mfupi sana kufanya upigaji kura na haikuwezesha ushiriki wa kutosha wa umma.

Baadhi ya mataifa ya Afrika kama vile Uganda yameharamisha mapenzi ya jinsia moja
Baadhi ya mataifa ya Afrika kama vile Uganda yameharamisha mapenzi ya jinsia moja AP

Sheria hiyo, wanasema, pia inakiuka haki na uhuru wa kikatiba ikiwa ni pamoja na haki ya usawa na kutobaguliwa, haki ya uhuru wa kujieleza na kujumuika.

Mnamo Agosti, mwanamume mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mtu wa kwanza kufunguliwa mashitaka kwa ulawiti uliokithiri na huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema watu wameteswa, kupigwa, kukamatwa na kufukuzwa katika maeneo yao kwa sababu ya kuhusishwa na wapenzi wa jinsia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.