Uganda: Mfalme wa Rwenzururu, Charles Wesley Mumbere arejea nyumbani
Nairobi – Mfalme wa kikabila nchini Uganda amerejea nyumbani kwa kukaribishwa kwa shujaa, miaka saba baada ya makumi ya watu kuuawa wakati wa uvamizi wa polisi kwenye ikulu yake.
Imechapishwa:
Umati wa watu wenye shangwe ulijitokeza katika mitaa ya Kasese kwa ajili ya kumpokea mfalme wa Rwenzururu, Charles Wesley Mumbere.
Mnamo mwaka wa 2016 alishtakiwa kwa kuwaamuru wanamgambo kutoka katika Ikulu yake kwa lengo la kuunda serikali yake huru inayojisimamia.
JUST IN: Rwenzururu king Charles Wesley Mumbere has arrived in Kasese for the first time in seven years since 2016 when his palace was raided by security operatives in November 2016.#MonitorUpdates
— Daily Monitor (@DailyMonitor) October 4, 2023
📸 @ALEXASHABA1 pic.twitter.com/4rp0xsxUH9
Serikali ya Uganda ilisema zaidi ya watu 100 waliuawa wakati wa operesheni hiyo ya polisi lakini mashirika ya kutetea haki ya binadamu yalisema watu wengi zaidi waliuawa.
Mfalme Mumbere na makumi ya wengine walikabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo uhaini, mauaji na ugaidi lakini waendesha mashtaka walifuta kesi hiyo baada ya kuomba msamaha.
The return of the Omusinga...
— NTV UGANDA (@ntvuganda) October 4, 2023
The Omusinga of Rwenzururu, Charles Wesley Mumbere has arrived in Kasese amid celebrations after an absence of about 7 years. #NTVNews pic.twitter.com/BkHeIjGej9
Ufalme wa Rwenzururu ni wa watu wa kabila la Bakonzo na una historia ya mielekeo ya kujitenga na mivutano ya muda mrefu na serikali ya Uganda.