Pata taarifa kuu

Uganda: Polisi wamezuia shambulio la ADF: Rais Museveni

Polisi nchini Uganda limefanikiwa kuzuia kutokea kwa mashambulio ya mabomu yaliyokuwa yatekelezwe na kundi la kigaidi la ADF, Kilomita 50 kutoka jiji kuu Kampala.

Waasi wa ADF wamekuwa wakitekeleza mashambulio nchini DRC na baadhi ya maeneo nchini Uganda
Waasi wa ADF wamekuwa wakitekeleza mashambulio nchini DRC na baadhi ya maeneo nchini Uganda © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema mabomu wawili yalikuwa yametegwa kwenye makanisa katika maeneo ya Kibibi na Butambala, lakini maafisa wa polisi wakabaini mpango huo mapema na kuutegua.

Aidha, Museveni amesema maafisa wa usalama waliuawa, lakini hakueleza zaidi.

Kiongozi huyo amewataka raia wa nchi yake kuwa macho, akisema baada ya ADF kuendelea kushambuliwa katika nchi jirani ya DRC, wanaendelea kupanga kisasi kwa kutekeleza mashambulio ya bomu katika ardhi ya Uganda

Mwezi Septemba, polisi nchini Uganda walisema walifanikiwa kuzuia jaribio la kundi hilo kutekeleza shambulio ndani ya Kanisa moja jijini Kampala.

Waasi wa ADF wanaohusishwa na kundi la Islamic state walitekeleza shambulio kwenye shule nchini Uganda miezi kadhaa iliyopita
Waasi wa ADF wanaohusishwa na kundi la Islamic state walitekeleza shambulio kwenye shule nchini Uganda miezi kadhaa iliyopita AP - Hajarah Nalwadda

Hata hivyo, mwezi Juni ADF inayoshirikiana na kufadhiliwa na kundi la Islamic State kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa,  walishambulia Shule ya Sekondari, katika mpaka na DRC na kusabisha vifo vya watu 42 wakiwemo wanafunzi 37.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.