Pata taarifa kuu

DRC: CENI imepokea majina 24 ya wagombea urais kuelekea mchujo

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha kupokea orodha ya wagombea 24 wa urais ambao wamejisajili kuwania katika ucaguzi wa Desemba 20.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Dénis Kadima, ametangaza utaratibu wa wagombea kuwasilisha maombi ya kuwania nyadhifa mbalimbali kuelekea uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Dénis Kadima, ametangaza utaratibu wa wagombea kuwasilisha maombi ya kuwania nyadhifa mbalimbali kuelekea uchaguzi huo. © CENI DRC
Matangazo ya kibiashara

Licha ya orodha hiyo, wagombea bado wanahitaji kuidhinishwa na mahakama ya kikatiba kabla ya orodha kamili ya wagombea kuchapishwa tarehe 18 ya mwezi Novemba.

Rais Felix Tshisekedi, aliyeingia madarakani mwaka wa 2018, amewasilisha ombi la lake la kuwania katika uchaguzi huo mapema mwezi Oktoba, akiwania kuongoza DRC kwa awamu ya pili.

Tschisekedi, anawania katika uchaguzi huo kutafuta nafasi ya kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya pili
Tschisekedi, anawania katika uchaguzi huo kutafuta nafasi ya kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya pili AFP - LUDOVIC MARIN

Kutokana na kile ambacho kimetajwa kwa mgawanyiko katika muungano wa upinzani, Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60, amepewa nafasi ya kuibuka mshindi kwa mujibu wa mtaalam wa masuala ya kisiasa nchini humo Christian Moleka.

Upinzani wa kisiasa ambao umetajwa kugawanyika utahitaji kumuunga mkono  mgombea mmoja ili kupata nafasi ya kumshinda Tshisekedi, kulingana na Moleka.

Denis Mukwege, Mgombea wa urais nchini DRC
Denis Mukwege, Mgombea wa urais nchini DRC © Riccardo Savi / Getty Images via AFP

Wapinzani wakubwa wa Tshisekedi ni pamoja na mshindi wa Tuzo ya Nobel Dkt Denis Mukwege, mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa Katanga Moise Katumbi, na Martin Fayulu, mgombea ambaye hakufanikiwa mwaka wa 2018.

Mbunge Delly Sesanga na mawaziri wakuu wa zamani Adolphe Muzito na Augustin Matata Ponyo pia wako kwenye kinyang'anyiro hicho, wa pili wakikabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu.

Moïse Katumbi Mmiliki wa TP Mazembe ya nchini DRC na mgombea wa urais
Moïse Katumbi Mmiliki wa TP Mazembe ya nchini DRC na mgombea wa urais AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Kuna mwanamke mmoja pekee kati ya wagombea 24, Marie-Josee Ifoku Mputa, ambaye pia alishiriki katika uchaguzi wa 2018.

Hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa ya sintofahamu kwa miezi kadhaa, huku vyama vya upinzani vikidai kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa wazi.

Augustin Matata Ponyo, aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa DRC naye pia anawania
Augustin Matata Ponyo, aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa DRC naye pia anawania © Frederico Scoppa, AFP

Uchaguzi wa urais unafanyika pamoja na uchaguzi wa wabunge, mikoa na manispaa, ambao maelfu ya wagombea wamejiandikisha.

Adolphe Muzito naye pia anawania kwenye uchaguzi huo
Adolphe Muzito naye pia anawania kwenye uchaguzi huo AFP - EUGENE SALAZAR

Raia wa DRC wanatarajia kuwa kiongozi mpya atakayechaguliwa atasaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto za kiusalama katika eneno la mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.