Pata taarifa kuu

Uganda: Uingereza imeonya uwezekano wa kutokea shambulio la kigaidi

Nairobi – Ubalozi wa Uingereza nchini Uganda, umeonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulio la kigaidi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki ikwemo kuwalenga raia wa kigeni, hatua inayokuja saa chache baada ya ubalozi wa Marekani kutoa onyo kama hilo.

Mamlaka imesema imezuia mashambulio mawili tofauti ya kigaidi ya ADF waliokuwa wamelenga kushambulia makanisa mwezi Septemba na Oktoba
Mamlaka imesema imezuia mashambulio mawili tofauti ya kigaidi ya ADF waliokuwa wamelenga kushambulia makanisa mwezi Septemba na Oktoba AFP
Matangazo ya kibiashara

Ubalozi wa mataifa hayo mawili umewaonya raia wake kuepuka kuhudhuria mikusanyiko mikubwa ya hadhara ikiwemo katika maeneo ya ibaada.

Aidha mataifa hayo pia yamewataka raia wake kutohudhuria tamasha maarufu la muziki la Nyege Nyege siku ya Alhamis.

Serikali ya Marekani pia imetoa wito kwa raia wake kutotembelea mbuga ya wanyama ya Semuliki na ile ya kitaifa ya Queen Elizabeth pamoja na mbuga nyengine za kitaifa.

Raia wa Uingereza na wanandoa wawili wenye asili ya Afrika Kusini pamoja na muongozaji wao raia wa Uganda waliuawa wiki iliyopita na watu wanaotuhumiwa kuwa waasi wa ADF katika mbuga ya wanyama ya Queen Elizabeth.

Uganda imekuwa ikiimarisha usalama wake katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Mamlaka imesema imezuia mashambulio mawili tofauti ya kigaidi ya ADF waliokuwa wamelenga kushambulia makanisa mwezi Septemba na Oktoba.

Mwezi Juni, waasi wa ADF waliwaua wanafunzi 42 kwenye shule Magharibi mwa Uganda, mojawapo ya mashambulio mabaya zaidi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.