Pata taarifa kuu

DRC : Matata Ponyo kumuunga mkono Moise Katumbi kuwania urais

Nairob – Aliyekuwa waziri mkuu wa DRC Matata Ponyo, ameamua kujiondoa katika kinyanganyiro cha urais mwezi ujao na badala yake ametangaza kumuunga mkono gavana wa zamani wa eneo la Katanga, Moise Katumbi.

Ponyo anasema anaamini wanasiasa wengine wa upinzani watafuata mfano wake na kujiondoa kwenye uchaguzi huo ilikumuunga mkono Moise Katumb
Ponyo anasema anaamini wanasiasa wengine wa upinzani watafuata mfano wake na kujiondoa kwenye uchaguzi huo ilikumuunga mkono Moise Katumb © Frederico Scoppa, AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita wagombea wa upinzani katika uchaguzi huo, Denis Mukwege, Delly Sesanga, Moïse Katumbi na Matata Ponyo, waliamua mjini Pretoria, Afrika Kusini, kuunda muungano mpya wa kisiasa, unaoitwa Congo ya Makasi.

Ponyo anasema anaamini wanasiasa wengine wa upinzani watafuata mfano wake na kujiondoa kwenye uchaguzi huo ilikumuunga mkono Moise Katumbi.

Moise Katumbi ni gavana wa zamani na jimbo la Katanga
Moise Katumbi ni gavana wa zamani na jimbo la Katanga REUTERS - Kenny Katombe

Katumbi na Ponyo, walifanya kazi katika serikali ya rais wa zamani Joseph Kabila ambapo Ponyo alihudumu katika wadhifa wa waziri mkuu kwa kipindi cha miaka mine.

Katika upande mwengine, Katumbi alikuwa gavana wa jimbo la Katanga kwa kipindi cha miaka tisa.

Rais Tshisekedi, anayewania kuongoza DR Congo kwa muhula wa pili, ni miongoni mwa wagombea waliozindua kampeni zao hapo jana Jumapili kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba.

Augustin Matata Ponyo na Mosie Katumbi walifanya kazi katika serikali ya Joseph Kabila katika nyadhifa tofauti.
Augustin Matata Ponyo na Mosie Katumbi walifanya kazi katika serikali ya Joseph Kabila katika nyadhifa tofauti. © AFP - FEDERICO SCOPPA

Ni kampeni zinazotazamwa si tu na raia wa Congo lakini jumuiya ya kimataifa na waangalizi wa uchaguzi, ambao wametoa wito wa amani licha ya eneo la mashariki kukabiliwa na utovu wa usalama, hali inayozua maswali ikiwa baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo yatafanya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.