Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Wanajeshi wa Uganda wameondoka katika kikosi cha Afrika Mashariki kilichopo DRC

Wanajeshi wa Uganda "wamevuka mpaka wa Bunagana na kuingia Uganda baada ya kuondoka katika eneo la misheni nchini DRC," jeshi la Uganda limetangaza katika taarifa, bila kutaja idadi ya wanajeshi. "Tumerudisha majeshi yetu nyumbani na tunaamini kuwa tumefikia malengo ya misheni," msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye ameliambia shirka la habari la AFP.

Wanajeshi wa Uganda kutoka kikosi cha kikanda cha EAC waliotumwa Bunagana, DRC, Aprili 2023.
Wanajeshi wa Uganda kutoka kikosi cha kikanda cha EAC waliotumwa Bunagana, DRC, Aprili 2023. AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi kutoka jeshi la Afrika Mashariki walianza kuwasili Goma mnamo mwezi wa Novemba 2022, takriban mwaka mmoja baada ya kuibuka katika mkoa wa Kivu Kaskazini uasi wa M23 ("March 23 Movement") ambao, kwa kuungwa mkono na Rwanda kulingana na vyanzo vingi, wamechukua maeneo makubwaya mkoa huo.

Kisha mamlaka ya Kongo iliitaka EAC kupeleka jeshi lake kukomboa maeneo yaliyotekwa na waasi. Lakini Wakongo haraka wakawalaumu sana wanajeshi wa EAC, wakiwashutumu kwa kushirikiana na waasi badala ya kuwalazimisha kuweka silaha chini. Kinshasa, ikiona kwamba kikosi hicho hakifanyi kazi, ilitangaza mwezi uliopita kwamba haitaki kuongeza mamlaka yake ifikapo Desemba 8. Kuchukua nafasi hiyo, DRC inategemea hasa wanajeshi kutoka Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Kuondoka kwa kikosi hicho cha kikanda kunakuja huku mapigano yakiendelea kati ya M23 na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na wanamgambo wanaojiita "wazalendo". Makundi mengi yenye silaha na wanamgambo wengine wameendelea kwa miongo mitatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, urithi wa vita vya kikanda ambavyo vilizuka katika miaka ya 1990 na 2000.

Uchaguzi mkuu, ambapo Rais anayemaliza muda wake Félix Tshisekedi atawania, umepangwa kufanyika Desemba 20. Kwa sababu ya uasi wa M23, hautafanyika katika maeneo mawili ya mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.