Pata taarifa kuu

Rais Ndayishimiye asema wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wapigwe mawe

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye katika mkutano na waandish wa Habari, amesema watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini humo wanapaswa kupigwa mawe, kitendo ambacho amesema hakitakuwa cha kihalifu.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye AP - Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Aidha, ameyataka mataifa tajiri kubaki na misaada yao iwapo, itaambatana na masharti ya kuitaka Burundi kuunga mkono vitendo na mapenzi ya jinsia moja.

Ndayishimiye, ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki, ameelezea mapenzi ya jinsia moja kama suala lisilokubalika.

"Binafsi hao watu wakionekana nchini Burundi, tunapaswa kuwapeleka uwanjani na kuwapiga mawe. Hii haitakuwa dhambi kwa watakaofanya hivyo," alisema wakati akiwahotubia raia wa nchi yake.

Kiongozi huyo wa Burundi, amewataka pia Warundi wanaoishi nje ya nchi waliochagua kujihusisha na vitendo hivyo, wasirudi nchini humo.

"Warundi wanaoishi nje ya nchi waliochagua maisha ya kishetani wasirejee,” aliongeza.

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ni haramu katika nchi za Afrika Mashariki, na mwezi Mei, nchi jirani ya Uganda ilipitisha sheria kali, inayopambana na vitendo hivyo.

Hatua hiyo ya Uganda imelaaniwa na Marekani ambayo imeiondoa kwenye ushirikiano wa kibiashara huku Benki ya dunia, ikisitisha kutoa mikopo kwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.